Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 11:26 pm

NEWS: WAZIRI LUKUVI AZINDUA LESENI YA ARDHI YA KIELETRONIKI

Dar es salaam: Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi amezindua rasmi mpango wa kutambua na kusajili kila sehemu ya ardhi kwa njia ya Kieletroniki kwa Mkoa wa Dar es Salaam kama sehemu ya kuongeza usalama wa milki ya ardhi hapa nchini

Akizungumza jana Machi 16,2019 wakati wa uzinduzi wa mpango huo ambao utaanza kwa Mkoa wa Dar es Salaam na kisha kuendelea mikoa yote nchini, Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amesema leseni hiyo baada ya kutolewa itadumu kwa miaka mitano.

“Ndani ya hii leseni ya kieletroniki ambayo itadumu kwa miaka mitano kutakuwa na taarifa zote muhimu.Kutakuwa na jina la mmiliki wa ardhi, ukubwa wa kiwanja, majirani zake, namba za kitambulisho cha Taifa na taarifa nyingine muhimu. “Kwa hiyo leseni hiyo ya makazi itawezesha kila kipande cha ardhi kutambuliwa kikamilifu, hata ukiwa nje ya Tanzania kiwanja kitaonekana maana kipo kieletroniki. “Tutaondoa changamoto za ujambazi wa viwanja lakini pia wakati huo huo leseni ya makazi itasaidia katika kupata mkopo benki na leseni hii itarahisisha masuala ya ulinzi na usalama,”amesema Lukuvi.

Amesema kila mwananchi atatakiwa kuchangia Sh.5000 ambapo Sh.4000 zitakwenda katika manispaa na Sh.700 itakwenda kwa kijana ambaye ni mtaalama anayetembea na simu kwa ajili ya kufanya usajili huo na Sh 300 zitakwenda kwa Mwenyekiti wa Serika

Amesema leseni hizo mpya ni muhimu na kutoa ufafanuzi kwa Mkoa wa Dar es Salaam ni muhimu kuwa nazo kwani leseni za makazi zilizokuwepo zimekwisha muda wake maana ni za mwaka mmoja mmoja tu. “Sheria ya makazi inaeleza wazi walioko kwenye maeneo ambayo hayajapimwa na yapo kiholela badala ya kubomoa makazi yao yanatakiwa kuboreshwa.Nia ya Serikali ni kuhakikisha watu wanaishi kwa usalama katika makazi yao, kikubwa tunaomba ushirikiano kufanikisha mchakato huu.Hatutatoka Dar es Salaam hadi pale ambapo tutaona tumemaliza kazi,”amesema Lukuvi.