Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 5:36 pm

NEWS: WAZIRI LUKUVI AMSIMAMISHA KAZI AFISA ARDHI KIGAMBONI

Dar es Salaam. Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi nchini Tanzania, William Lukuvi leo ametekeleza agizo la Rais Magufuli la kumsimamisha kazi afisa ardhi wa Wilaya ya Kigamboni.

Siku tano zilizopita Rais John Magufuli alitaka alimlalamikia Afisa Ardhi huyo na akataka achukuliwe hatua kwa kuwa haonekani kazini kwa muda sasa.

Lukuvi ametoa maamuzi hayo leo Jumatatu Februari 17, 2020 wakati akikabidhi ekari 715 za ardhi kwa manispaa ya Kigamboni kama alivyoagizwa na Rais Magufuli wakati akizindua ofisi za mkurugenzi, mkuu wa wilaya ya Kigamboni pamoja na hospitali ya wilaya hiyo.

Siku hiyo Magufuli alisema, “nina tatizo na ofisa ardhi wa Kigamboni ni mtoro na hajafanya kazi karibu miezi mitatu, aliandikiwa barua na Wizara ya Ardhi ili ashughulikiwe ila bado wizara wanaleta mshahara wake. Najua wizara watafikishiwa ujumbe, kama ni mtoro atoroke kabisa, sifahamu mkurugenzi mmechukua hatua gani kwa ofisa ardhi huyo ambaye hafanyi kazi.”

Katika maelezo yake ya leo, Lukuvi amesema mtumishi huyo amesimamishwa kazi.

"Bahati nzuri tulishapata barua kutoka kwa mkurugenzi wa Kigamboni na tumeshamsimamisha kazi wakati hatua za kinidhamu zikiendelea .Kama kutakuwa na uhitaji tutaleta mtu mwingine," amesema Lukuvi.