- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WAZIRI LUGOLA NA MUSIBA WAVIMBIANA
Dodoma. Waziri wa Mambo ya Ndani nchini Tanzania, Kangi Lugola amemuonya Cyprian Musiba anayejiita kama mwanaharakati anayemtetea Rais Magufuli akimtaka kuacha tabia ya kuwachafua viongozi na watu mbalimbali kwa madai kuwa ametumwa na Serikali ama Rais.
Lugola ametoa kauli hiyo leo Ijumaa Septemba 13, 2019 katika mkutano wake na waandishi wa habari mjini Dodoma, kusisitiza kuwa Musiba akiendelea atachukuliwa hatua kali za kisheria.
Waziri huyo amesema Musiba amekuwa akiwachafua baadhi ya viongozi na wananchi kwa madai kuwa ni mtetezi wa Rais Magufuli na kuwaaminisha watu kuwa anatumiwa na Serikali, jambo alilodai kuwa si kweli.
Lugola amesema Serikali haina mpango wa kuwatuma wanaharakati, haimtumii Musiba kuwaumiza watu akimtaka kufanya shughuli zake bila kutumia mgongo wa Serikali.
Muda mchache mara baada ya Waziri Lugola kumuonya Mwanaharakati huyo Musiba ameliambia gazeti la Mwananchi na kusema kuwa yupo tayari kukamatwa, kuwekwa mahabusu au kufungwa jela lakini hatoacha kumsemea Rais wa Tanzania, John Magufuli.