- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WAZIRI LUGOLA AHIDI KUMKAMATA KIGOGO
Dar es Salaam. Waziri wa Mambo ya Ndani nchini Tanzania, Kangi Lugola amesema siku za mtu anayejiita mwanaharakati wa haki za binaadamu na mkosoaji mkubwa wa Serekali nchini Tanzania 'Kigogo' zinahesabika.
Kigogo ni utambulisho wa jina linalotumiwa na mtu katika mitandao ya kijamii haswa Twitter akiwa anajikita haswa kwenye maswala ya Ukosoaji wa Serekali ya Rais Magufuli na Vyama vya Siasa.
Lugola ametoa kauli hiyo leo Jumamosi Novemba 2, 2019 katika mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika jijini Dar es Salaam wakati akitoa ufafanuzi kuhusu makosa ya mtandao.
“Kuna mtu anayejiita Kigogo kwenye mtandao wa Twitter kazi yake kubwa ni kuikosoa Serikali katika mambo mbalimbali, nasema siku zake zinahesabika,” amesema Lugola.
Lugola amesema kama ilivyo kalenda, hata siku za mtu huyo zinahesabika, akibainisha kuwa atakamatwa.