- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WAZIRI LUGOLA AFUNGUKA KUHUSU WATU WASIOJULIKANA KUTEKWA.
DODOMA: Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amezionya baadhi ya asasi za kiraia ambazo zimekuwa na tabia ya kuitukana Serikali pamoja na kusema kwamba hakuna jambo lolote ambalo limefanywa na Serikali hiyo.
Waziri Lugola alitoa kauli hiyo leo Jijini hapa, wakati wa uzinduzi wa Ofisi ya Kituo cha Haki za Binadamu (LHRC) Mkoani Dodoma ambao ulienda sambamba na kampeni ya miaka 25 ya Kituo hicho na uzinduzi wa tuzo ya Majimaji ambayo hutolewa kwa mtu ambaye ametoa mchango mkubwa wa kisheria katika jamii.
Waziri Lugola amesema Serikali imebaini kuna asasi zisizokuwa za kiserikali ambazo zinaitukana Serikali pamoja na kusema kwamba hakuna jambo lolote ambalo limefanywa na Serikali hiyo.
“Siku za hivi karibuni tumebaini kuwepo kwa asasi zisizo za kiserikali ambazo zinatumia mwanya wa kukosoa Serikali lakini wanaenda mbali badala ya kukosoa serikali wanaitukana Serikali na wanaenda mbali kuipotosha jamii na wengine wakisema Serikali ya awamu ya tano haijafanya kitu,"amesema.
Alisema uanaharakati wa namna hiyo hauitendei haki Serikali ya awamu ya Tano kwani Serikali ya awamu ya tano imefanya mambo mengi ya maendeleo na inaendelea kufanya, hivyo si vyema kusema kwamba Serikali haijafanya kitu.
Pia Kangi ambaye ni Mbunge wa Mwibara(CCM), alisema kumekuwa na sintofahamu kwenye suala la haki na Serikali imebaini kwamba inapotokea haki kuminywa ndipo mlipuko wa kwamba kuna uvunjika kwa haki za binadamu unapotokea.
“Haki huambatana na wajibu,hivyo ni vyema tunapohubiri haki za binadamu tuhubiri na wajibu huo, kila raia katika kuhakikisha anatimiza wajibu wake kwa njia zenye kuthamini utu na utaifa letu.
Amesema anatamani siku moja lianzishwe Shirika lisilokuwa la kiserikali linalohubiri na kutetea suala la haki na wajibu kwa Watanzania
“Tumebaini kwamba inapotokea kuminywa kwa haki ndipo unapotokea mlipuko wa kuashiria kuwa kuna uvunjifu kwa haki za binadamu umetokea, ukumbuke ikitokea raia asitimize na kutekekeleza wajibu wake na penyewe patatokea mlipuko kwa kuvunja haki za binadamu,” amesema Lugola.
Waziri huyo amesema tangu kituo hicho kimeanzishwa kimeendelea kuwa kimbilio la wanyonge kwa kuzidi kuwa cha kipekee katika utetezi nchini.
“Serikali imeendelea kutoa fursa kwa asasi kuendelea kufuatilia masuala mbalimbali kwa mujibu wa Katiba,kituo cha sheria na haki za binadamu kimekuwa kiungo muhimu baina ya raia na serikali yao,”amesema.
Waziri Lugola amefafanua kuwa mpaka sasa hivi hajapokea rufaa ya mtu yoyote kuonewa licha ya wengi kupiga kelele kwamba wamekuwa wakionewa.
“Tangu nimepewa dhamana hii sijawahi kupokea rufaa yoyote,nataka rufaa nazisubiri rufaa haziji,”amesema.
Kuhusu watu kutekwa na kuuwawa, Waziri Lugola amesema, amewataka watanzania kusonga mbele na kwamba kama kuna mtu kapotea Serikali ipo, Jeshi la Polisi linafanya kazi vizuri na hilo wamelisema sana hivyo hapendi kulirudiarudia na kusisitiza kuwa Serikali inapaswa kuheshimiwa.
Kwa upande wake,Mkurugenzi wa Kituo cha Haki za Binadamu Nchini (LHRC) Anna Henga alisema kuzindua ofisi hiyo Dodoma ni kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya tano ya kuhamishia Serikali Mkoani humo.
“Tunafurahi sisi kuwa kimbilio la watu wengi wenye kuhitaji msaada kubwa tumeendelea kubadili mitazamo kwa kuheshimu misingi ya haki za binadamu na sisi ni kimbilio la wanyonge,” amesema Anna.