Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 6:31 am

NEWS: WAZIRI KAMWELWE AVUNJA BODI YA MFUKO WA BARABARA NA KUUNDA MPYA

WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe, ameivunja Bodi ya Mfuko wa Barabara nchini na kuunda mpya, ambayo itaendesha mfuko huo kwa miaka mitatu ijayo.

Image result for Isack Kamwelwe na waandishi

Waziri Kamwelwe alifanya uamuzi huo juzi kutokana na kumaliza muda wake. Kwa mujibu wa sheria, wajumbe wa bodi hiyo wanatakiwa kukaa madarakani kwa miaka mitatu na wanaweza kuongezwa kipindi kingine cha miaka mitatu na baada ya hapo wanafikia kikomo.

Baada ya kuunda bodi mpya, Kamwelwe aliiagiza kuhakikisha inasimamia vizuri mfuko huo ikiwamo kuhakikisha miradi yote inayotekelezwa inakuwa na thamani halisi ya fedha zinazotolewa.

Alisema barabara nyingi nchini zinakabiliwa na changamoto ya uharibifu wa miundombinu yake ikiwamo wizi wa alama za barabarani, umwagaji wa mafuta ambayo yanasababisha ajali na kupitisha mizigo mizito kuzidi uwezo wa barabara.

Image result for Isack Kamwelwe na waandishi

yapite huko na tupunguze ajali,” alisema Kamwelwe. Aidha, aliitaka bodi hiyo kuanza kutekeleza mradi huo katika mwaka wa fedha 2019/2020 na ndani ya mwezi mmoja kuanzia sasa impatie taarifa ya utekelezaji wake.

Katika hatua nyingine, Waziri Kamwelwe alitoa siku 14 kwa Wakala wa Barabara (Tanroads) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi kuwalipa fidia wananchi wa Mji wa Kasumulu wilayani Kyela wanaotakiwa kupisha mradi wa ujenzi wa kituo cha pamoja cha forodha kati ya Tanzania na Malawi.

Alisema Rais John Magufuli aliagiza wananchi hao walipwe tangu Mei mwaka huu, lakini anashangaa mpaka sasa hawajalipwa licha ya fedha za kuwalipa kuwa tayari zimeshaingizwa kwenye mfuko wa Tanroads.

“Nilitaka niwape siku tatu kuwalipa wananchi hao, lakini kwa sababu ni masuala yanayohusu fedha nawapa mpaka kufikia Agosti 10 muwe mmewalipa wote na atakayekwamisha tutaonana,” alisisitiza Mhandisi Kamwelwe.