- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WAZIRI KAMWELWE ATISHIA KUMFUTA KAZI MKURUGENZI TPA
Dar es Salaam. Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano nchini Tanzania Isack Kamwelwe ametishia kumfuta kazi Mkurugenzi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) Deusdedit Kakoko Kama hata ongeza gawio kwa Serikali kutoka Sh480 bilioni la mwaka huu hadi Sh1 trilioni mwaka 2019/20.
Waziri Kamwelwe ametoa agizo leo Jumamosi Desemba jana 21, 2019 katika uzinduzi wa bodi mpya ya mamlaka hiyo yenye wajumbe saba ikiongozwa na Profesa Ignas Rubaratuka aliyeteuliwa kwa mara ya pili.
Waziri Kamwelwe amesema haridhishwi na ukusanyaji wa kodi bandarini, kuitaka bodi hiyo kulifanyia kazi eneo hilo na kuhakikisha TPA inakusanya kodi na kuongeza gawio lake serikalini.
“Ikitokea leo Rais John Magufuli ananifukuza kazi kwa sababu ya TPA kushindwa kukusanya kodi vizuri, binafsi sitotetereka sana kwani nitaendelea kuwa mbunge, ila nyinyi ndio mtaathirika zaidi,” amesema waziri huyo.
Akizungumzia bodi hiyo, Profesa Rubaratuka amemhakikishia Kamwelwe kuwa watafanya kazi kikamilifu.
“Bodi kwa kushirikiana na wafanyakazi na wadau wengine, itahakikisha lengo la kutoa gawio la Sh1 trilioni linafanikiwa,” amesema Profesa Rubaratuka.