- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WAZIRI KALEMANI AIPA SIKU 30 TANESCO KUPELEKA UMEME SINGIDA MASHARIKI
WAZIRI wa Nishati, Dk. Medard Kalemani ameliagiza Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Mkoa wa Singida kuhakikisha ndani ya mwezi mmoja wanapeleka umeme katika vijiji 11 vilivyopo Jimbo la Singida Mashariki.
Pia Waziri Kalemani ameiagiza Tanesco Singida kuhakikisha wanamsimamia mkandarasi aanze kusimika nguzo mapema katika Tarafa ya Mungaa Lighwa, Ntuntu,Misughaa na Kikio ili umeme uwashwe kwenye Vijiji kabla ya Juni, mwaka huu
Dk. Kalemani alitoa maagizo hayo jana Aprili 19, 2020 wilayani Ikungi akiwa katika ziara ya kukagua miradi ya umeme ambapo amewasha umeme katika vijiji viwili vya Matare na Nkuhi.
“Nampongeza sana Mbunge wenu Miraji Mtaturu, kwani anafuatilia sana miradi ya wananchi wake, tangu amechaguliwa na kuapishwa ni miezi mitano tu lakini mnaona mambo yalivyo, tumewasha vijiji viwili je angekaa miaka minne hali ingekuwaje?,” alihoji Dk. Kalemani.
Akizungumzia ugonjwa wa corona, alisema kuwa isiwe sababu ay kusimama kwa kazi ya miradi ya umeme nchini.
“Ndugu zangu ugonjwa huu wa homa kali ya mapafu unaosababishwa na virusi vya Corona (COVID 19) usikwamishe kazi za kuunganishia umeme wananchi ila mfanye kazi kwa tahadhari,tutaendelea kukagua miradi ya umeme kila mahali kwa kuwa wananchi wanahitaji umeme na Rais Dk. John Magufuli ameidhinisha Shilingi bilion 40 kwa Mkoa wa Singida ili kutekeleza miradi hii hivyo ni lazima tuisimamie,” alisema Dk. Kalemani.
Pamoja na hayo Dk. Kalemani amesisitiza wananchi kutolipishwa nguzo na gharama za kuunganishiwa umeme amesema ni Sh 27,000 na sio vinginevyo.
“Katika hili niagize hapa mkandarasi wa Cyba Contractors Ltd ya Jiji Mbeya aliyelalamikiwa kuwatapeli wananchi baada ya kuchukua pesa zao na hajafanya wiring mpaka sasa atafutwe,” alisema
Awali akizungumza katika ziara hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Edward Mpogolo alisema katika kata 28 zilizopo wilayani humo ni kata 18 tu ndio zimefikiwa na umeme hivyo kumuomba waziri aendelee kuwasaidia.