- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WAZIRI JAFO ATOA MWEZI MOJA KWA HALMASHARI ZOTE NCHINI.
DODOMA: Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Selemani Jafo ameagiza ifikapo Novemba 30 mwaka huu halmashauri zote nchini ziwe zimefungua akaunti maalum ya fedha za mfuko wa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.
Jafo ametoa agizo hilo jijini Dodoma wakati akifunga kongamano la wa wataalam wa maendeleo ya jamii na kumtaka katibu mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI kushirikiana na wizara ya fedha ili kutekeleza agizo hilo.
Waziri Jafo amesema takwa la fedha hizo kuwa na akaunti maalum kwa halmashauri zote 185 ni la kisheria wala si la hiari na kwamba itasaidia udhibiti wa fedha hizo kutotumika kwenye miradi mingine.
“Katika wafanyakazi ambao wamekuwa hawapewi kipaumbele na kudhalauliwa katika maeneo yao ya kazi ni wataalam wa maendeleo ya jamii lakini sasa wakati umefika kuwapatia vitendea kazi na kuwatumia katika shughuli zote za maendeleo ya Taifa”. Aliongeza Waziri Jaffo.
Aidha Waziri Jafo aliongeza kuwa kwa kipindi kirefu wataalam hawa wamekuwa hawatumiki ipasavyo na badala yake wamekuwa wakitumiwa wakati wa dharula au katika kazi za zimamoto wakati ukiangalia watumishi wengi wa serikali wataalam hawa ni moja ya kada yenye wasomi wengi.
Kufuatia ari hiyo waziri Jafo ameagiza mamlaka zilizochini ya Serikali za mitaa Nchini kuboresha mazingira ya kufanyia kazi ya wataalam wa sekta ya maendeleo ya jamii kwa kuwapatia vitendea kazi ikiwemo kuhakikisha wanapatiwa magari ili waweze kufuatilia kazi zao vizuri tofauti na sasa ambapo mazingira yao ya kazi yana hali duni.
Waziri Jafo pia amewataka wataalam hao wa maendeleo ya jamii kujiamini katika utendaji kazi wao na kuhakikisha wanasimamia misimamo katika vikao vya mbalimbali vya maamuzi ikiwemo CMT ili waweze kukubalika na kuaminika kama ilivyo kada nyingine katika maeneo yao ya kazi.
Waziri huyo amewaagiza watendaji kazi wote serikalini kufanya kazi kwa bidii ili hata mtumishi akienda likizo wanaobaki ofisini waone umuhimu wake lakini kama mtumishi akiama au kwenda likizo na watu wasione upungufu wowote ujue mtumishi huyo hatoshi katika eneo hilo.
Awali akimkaribisha mgeni Rasmi Katibu Mkuu Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu amesema kuwa kongamano la wataalam wa maendeleo wa jamii limekuwa na mada ambazo kimsingi zitawaletea mabadiliko katika utendaji kazi wao ikiwemo mada ya kuamsha ari ya wananchi kuoresha makazi yao.
Dkt Jingu amesema kongamano hilo limekuja na maadhimio na mapendekezo yanayoangazia namna bora ya utendaji kazi wao lakini kutokana na kongamano hilo wataalam hawa wamejiwekea malengo yanayopimika kwa mstakabali wa taaluma yao.
Wataalamu wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii wamekutana Jijini Dodoma katika Mkutano Mkuu wao wa mwaka kwa lengo la kukumbushana majukumu yao lakini pia kupata maarifa mapya kutoka mada mbalimbali zitakazotolewa katika mkutano huo wa siku nne.