November 26, 2024, 3:40 pm
- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WAZIRI HATARINI KUUBWAGA UWAZIRI KWA TUHUMA ZA RUSHWA
Dodoma: Mbunge wa Ndanda (Chadema), Cecil Mwambe amesema yupo tayari kuwasilisha ushahidi wote bungeni unaodhibitisha kuwa Naibu Waziri wa Viwanda, na Biashara Mhandisi Bi Stella Manyanya amehusika katika vitendo vya kuomba rushwa.
Kauli hiyo ya Mwambe ameitoa Leo Mei 17, 2019.
Mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge amemtaka Mbunge huyo kuwasilisha ushahidi bungeni Jumatatu 20/5/2019
Awali Naibu Waziri wa Viwanda, Mhandisi Stella Manyanya alisimama kuomba mwongozo wa Spika kuhusu tuhuma dhidi yake zilizotolewa na Mbunge Cecil Mwambe, ambapo Naibu Waziri Manyanya alieleza kuwa kama kweli ikithibitika amehusika na vitendo vya rushwa yupo tayari kuwajibika.