- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WAZIRI GWAJIMA AAGIZA UFUATILIAJI MAPATO YA HOSPITALI
TABORA. Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima amewaagiza viongozi wa hospitali zote nchini kuanzia ngazi ya Taifa, Mkoa, Wilaya kuunda Kamati ndogo ndogo za ufuatiliaji wa mapato ya fedha za uchangiaji kila siku toka vitengo vyote ili kufahamu bayana kiasi kinachokusanywa maana imebainika viko vitengo ambavyo makusanyo yake ya fedha za uchangiaji ni madogo kuliko kilichochangiwa au kilichotarajiwa kuchangiwa.
Ameelekeza Kamati hizo pia zihusike na kuchambua iwapo matumizi ya kwenye eneo la dawa na vipimo au bidhaa za afya kiwango kinafikia asilimia 50 au zaidi kama ilivyoelekezwa kwenye mwongozo wa wizara.
Dkt. Gwajima ametoa maagizo leo wakati akizungumza na watumishi wa Hospitali ya Rufaa Mkoa Kitete Mjini Tabora ambapo amesema kuwa iundwe Kamati hiyo ndogo ya kusimamia mapato ya fedha ili kudhibiti upotevu wa fedha za umma na utumiaji wa kiasi kidogo cha fedha za uchangiaji kwenye kununua bidhaa afya ikiwemo dawa.
Dkt Gwajima amesema kuwa usimamizi mzuri wa wa uendeshaji wa vituo kwa ujumla wake pamoja na usimamizi mzuri wa uwajibikaji kwenye matumizi ya raslimali zote ikiwemo fedha ni muhimu na ni chachu katika kuboresha huduma na kuvutia wateja wa makundi yote ya uchangiaji huduma ili dhana ya uendelevu wa huduma kwa uchangiaji na hususan Bima za Afya itimie kwa ukamilifu wake.