- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WAZIRI BASHUNGWA AZITAKA TAASISI KUTENGENEZA MIPANGO WEZESHI .
DODOMA: Waziri wa viwanda na biashara Innocent Bashungwa amezitaka taasisi zilizo chini ya wizara hiyo kutengeneza mipango wezeshi ambayo itasaidia kututoa hapa tulipo na kutufikisha katika uchumi wa viwanda, mipango ambayo haitakuwa kandamizi kwa wawekezaji.
Sambamba na kujenga uhusiano mzuri baina ya taasisi hizo na wenye viwanda na wafanya biashara ili kwa pamoja kuona changamoto ambazo zinawakabiri wafanyabiashara ambazo ni kikwazo kufikia malengo.
Ameyasema hayo jijini Dodoma wakati wa kikao kazi baina ya wakuu wa taasisi kumi na sita (16) pamoja na bodi zilizochini ya wizara hiyo, waliokutana kwa siku mbili Dodoma kujadili mbalimbali na namna ya kufikia walengo ya serikali.
Amezitaka taasisi hizo kuja na mbinu ambazo zitasaidia kuinua sekta hiyo bila kuathiri wawekezajina kukaa na wawekezaji kubaini changamoto mbalimbali ambazo wanakabiliana nazo katika kutekeleza majukumu yao.
“Lengo la kikao hiki ni kukaa na taasisi zetu ili kuona namna bora ya kufikia malengo tuliyojiwekea na mambo ambayo ni kikwazo katika kutekeleza,sasa niwatake taasisi msiwe kikwazo kwa wawekezaji, mtengeneze mipango ambayo itasaidia kututoa hapa tulipo na mipango ambayo haitakuwa kikwazo kwa wawekezaji” amesema Bashungwa.
Ametolea mfano kwa shirika la viwanda Tanzania TBS kuhakikisha bidhaa zinazozalishwakuwa na viwango, pia katika kudhibiti viwango wahakikishe hawaathiri wala kuchelewesha shughuri za mwekezaji.
Amesema katika kikao ambacho Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli alikaa na wafanyabiashara ikulu kilimpa mwanga namna ya kuja kufanya kazi ndani ya wizara hiyo na atahakikisha anasimamia kikamilifu wizara hiyo.
Amesema matokeoya kikao hicho tayari yameanza kuonekana ambapo kodi na tozo zilizokuwa kero zimeondolewa zaidi ya 54, amesema sambamba na hilo atahakikisha anafanya mageuzi katika sekta hiyo.
Pia amesema unaweza kufuta kodi hizo lakini tatizo likabaki palepale, amesisitiza kwenye taasisi kuimarisha mahusiano na wawekezaji na namna ya kuongea na wafanyabiashara, linaweza kuwa sida sio kero ya kodi bali ni mahusiano baina yao.
Amebainisha kuwa kuna haja ya kufungamanisha sekta ya kilimo na viwanda ili kuleta matokeo chanya katika wizara ya viwanda na biashara, na kuongeza kwa kusema kuna uhusiano mkubwa baina ya kilimo na viwanda hivyo vikifungamanishwa vinaweza leta matokeo mazuri.
Amesema ataimarisha mahusiano na Jumuiya ambazo Tanzania ni mwana chama kama EAC na SADC ili Kuweza kufaidika na kuwa wanachama kwa sababu Tanzania inalipa ada kila mwaka ni lazima ione matokeo yake na hasa katika sekta ya uwekezaji.
Kwa upande wake mwenyekiti wa bodi ya tume ya ushindani Humphrey shayo, amesema kikao hicho kilikuwa na faida kwa sababu kimezikutanisha taasisi kumi na sita(16) zilizo chini ya wizara hiyo na kujiona kumbe wanaweza kufanya jambo ila walikosa nafasi tu kama hiyo.
“Kikao kimekuwa kizuri taasisi zaidi ya 16 tumekutana jambo ambalo halijawahi kufanyika na kwa kikao hiki tumejiona kumbe tunaweza kufanya jambo ndani ya wizara hii” amesema.
Amesema wao kama tume ya ushindani wanafanya kazi kwa weledi mkubwa kwa kudhibiti bidhaa bandia kuingia nchini kwa kuhakikisha wanakagua makontena yote yanayoingia katika bandari.