Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 4:25 pm

NEWS: WAZIRI AWESO AMUWEKA NDANI MHANDISI WA MAJI WALAYA YA MKINGA

NAIBU Waziri wa Maji Juma Aweso ameliamuru Jeshi la Polisi wilayani Mkinga kumkatama Mhandisi wa Wakala wa Maji Vijiji (Ruwasa) wilaya ya Mkinga Castory Keneth kutokana na kushindwa kusimamia mradi wa maji wa Mbuta na kupelekea kushindwa kukamilika kwa wakati huku wananchi wakiendelea kutekeseka kupata huduma hiyo muhimu kwa maisha.

Mradi huo ulianza 2013 ambapo serikali ilitoa kiasi cha zaidi ya milioni 400 lakini utekelezaji wake ulishindwa kukamilika na kupeleke tatizo la maji kwenye eneo hilo ambalo kupata shida ya maji.

Hatua hiyo ilichukuliwa na Naibu Waziri huo mara baada ya kuutembelea mradi huo ambao ulikuwa ukitekelezwa na mkandarasi White City ya Jijini Dar es Salaam na serikali ilikuwa imekwisha kulipa zaidi y a sh.milioni 400 lakini hakuna kitu ambacho kimefanyika na mkandarasi huyo huku ameutelekeza.

Alisema wizara hiyo imebaba dhamana kubwa hivyo wataalamu msipokuwa makini mnaweza kuungiza kwenye matatizo na kuchukiwa na wananchi hivyo kuna haja ya pamoja kufanya mageuzi ya uzalishaji wa maji vijijini lakini lazima watipie wataalamu husika.

Naibu Waziri huyo alisema kwamba lazima Mkurugenzi Ruwasa ajiridhishe kwani wengine hawana sifa na kazi zao huku akimueleza kwamba mhandisi huyo hatoshi kwenye nafasi hiyo na hana uwezo ikiwemo kuwa na maslahi kwenye mradi huo.

“Hivyo Mimi kama Naibu Waziri nimeona kuna ubadhirifu mkubwa hapa hivyo nitatuma timu ya kuhakikisha ya mabwawa kuja kufanya tathimini kuona namna wanaweza kufanya kazi hii”Alisema

“Lakini wewe unatetea na kabisa inaonekana zahiri kuna fedha zimeliwa hapa sasa kabla hatujaenda huko nimuombe ODC akuchukua ukatusaidia kwenye jambo hilo”Alisema Naibu Waziri huyo.

Awali kabla ya kutoa maamuzi huyo Naibu Waziri huyo alimpa nafasi Mhandisi huyo wa Ruwasa kueleza kuhusiana na mradi huo na namna ulivyotekeleza ambapo alimueleza majibu yasiyoridhisha na kuamua kuchukua maamuzi hayo.

Hata hivyo serikali imesema kwamba kuhakikisha wannahi mkinga wanapata huduma ya maji kwa kuanzisha mamlaka ya maji pamoja na kupata mradi mkubwa utakaotoa maji Mabayani hadi Horohoro.

Awali akitoa taarifa ya wilaya hiyo kwa Naibu Waziri Aweso, Mbunge wa Jimbo la Mkinga (CCM) Dastan Kitandula alisema kwamba bwawa moja la mbuta lilishazolewa huku akikabidhiwa mkandarasi aanze kazi upya.

Alisema ilifikia mahali wakatumia ujanja ujanja kupasua tuta ili maji yasipasue tena tuta lakini eneo la Mwakijembe umejaa maji kwa hali hii yanaweza kutokea balaa wakati mwengine hivyo wanahitaji fedha haraka ili mkandarasi akamilishe mradi kwa sababu kazi ni ndogo.

Aidha alisema lakini wilaya ya Mkinga hawana mradi mkubwa wa maji hasa kwenye ukanda wa bahari eneo la mkinga mkoa wa Tanga ambapo ndio lina eneo kubwa kuliko sehemu nyengine na upozungumzia uwekezaji unaongeleo huku kuwepo mahoteli makubwa lakini hakuna wekezaji unauofanyika kutokana na ukosefu wa maji.

Hata hivyo alisema kwamba ule mradi wa mabayani ungeweza kutengewa fedha ufanyika kutoka Tanga mpaka horohro kilomita 65 na kinachoumiza maji wanayokunywa watu wa Jiji la Tanga chanzo chake ni Mkinga kata ya Bosha na Mhinduro wanatunza vyanzo vya maji lakini wao wanabaki watazamaji.

Naye kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Mkinga Yona Mark alisema kwamba wakazi wa wilaya hiyo wanapata maji bomba, visima na mabwawa kwa asilimia 56 ongezeko hilo ni asilimia mbili toka asilimia 54 2015/2016.

Alisema kwamba asilimia hiyo inatokana na kwamba wametengeneza mabwawa lakini hawajatengeneza miundombinu ya kuwapelekea wananchi maji kwenye maeneo yao .

Alisema wizara ya maji imewapelekea bilioni 2.9 ili kutekeleza miradi ya maji vijiji vya mapato,Makao Makuu ya wilaya ya Mkinga Parungu Kasera,Kilulu,Doda,Bwagamacho,Bamba Mavenegro,Mwarongo,Mbuta na Mwakijembe.

Mkuu huyo wa wilaya alisema kwamba ujenzi wa miradi ya maji vijijini walifanikiwa kupata vyanzo vya maji tisa badala ya kumi lakini vijiji saba vimekamilisha ujenzi huku miradi ya miwili ni ule wa Mbuta na Mwakijembe huku akieleza ule wa mbuta changamoto mkandarasi alikatisha mkataba kwa sababu kutokulipwa. Mwisho.