- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WAZIRI AMSIMAMISHA KAZI KIGOGO WA SHIRIKIA LA RELI TANZANIA
Morogoro: Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano nchini Tanzania Mhandisi Isack Kamwelwe ameagiza kusimamishwa kazi mara moja kwa Mkuu wa kitengo cha fedha wa Shirika la Reli nchini (TRC) Emmanuel Balele kutokana na kushindwa kuwalipa mshahara kwa muda mrefu, wafanyakazi wa reli wanaohusika kulinda na kukarabati kipande cha reli kilichozolewa na maji, maarufu kama pigilia, katika eneo la Msagala - Gulwe wilayani Kilosa Mkoani Morogoro.
Waziri Kamwelwe amefikia uamuzi huo baada ya kutembelea na kukagua maeneo yaliyoathirika na mafuriko yaliyosomba kipande cha reli ya kati inayotoka mikoa ya kanda ya ziwa hadi Dar es salaam, kipande cha zaidi ya kilometa 120 .