Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 3:45 am

NEWS: WAZIRI AIPA SIKU 30 TTCL KUSAMBAZA VOCHA NA LAINI ZAKE NCHI NZIMA

Dar es Salaam: Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Atashasta Nditiye amelipa muda wa mwezi mmoja kwa Shirika la Simu nchini Tanzania (TTCL) kuhakikisha maeneo yoote ambayo hayana kadi na vocha za simu za mtandao huo, zinapatikana ili wananchi wafaidi huduma zao.

Ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Februari 14, 2019 katika ziara ya kukagua utendaji kazi ya shirika hilo.

Amesema TTCL ni shirika la wananchi, hivyo wanapaswa kuona matunda yake moja kwa moja ikiwamo kupata huduma zake.

"Ninawapa mwezi mmoja kuitatua changamoto ya upatikanaji wa kadi na vocha kwenye maeneo ya vijijini na maeneo yote nchi mzima" amesema Nditiye.

Nditiye amefafanua kuwa shirika hilo limebuni vitu vingi vinavyopaswa kusimamiwa kikamilifu ikiwamo mkutano kwa njia ya video.

"Mbinu hii imekuwa rahisi na imepunguza gharama, kuna wakati waziri mkuu amekuwa akiwasiliana na mawaziri kwa njia hii, kutoa maelekezo na yanafanyiwa kazi,” amesema Nditiye.

"Msirudi nyuma endeleeni kubuni vitu vingine ili mlikamate soko la mawasiliano hapa nchini.”

Mwenyekiti wa bodi ya shirika hilo, Omary Nundu amesema wanataka kutumia miundombinu yao kufanya kazi.
“Changamoto zipo chache ambazo kimsingi zinafanyiwa kazi kuhakikisha zinamalizika, pia kuongeza matangazo ili wananchi watambue huduma zetu na kuzitumia, ”amesema Mhandisi Nundu.