Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 3:40 pm

NEWS: WAZIRI AIAGIZA TCRA KUICHUNGUZA MITANDAO YA SIMU INAYOWANYONYA WATUMIAJI

Serikali imetoa wiki mbili kwa Mamlaka ya mawasiliano tanzania TCRA kuzichunguza na kuzichukulia hatua stahiki baadhi ya kampuni za mitandao ya simu ya mkononi zinazoshutumiwa na wananchi kwa kukata ovyo vifurushi na wakiweka hela zinakwisha kabla ya muda wa matumizi .

Naibu Waziri wa uchukuzi na mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye ametoa kauli hiyo mara baada ya kuzindua mnara wa mawasiliano uliojengwa na kampuni ya simu ya Tigo katika kijiji cha Mavuji kata ya Mandawa wilayani Kilwa mkoani Lindi kufuatia malalamiko mengi aliyoyapokea kutoka kwa wananchi.