- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WAZEE JIMBO LA MTAMA WAAHIDI KUMCHUKULIA FOMU RAIS MAGUFULI
Wazee wa Jimbo la Mtama nchini Tanzania wameahidi kumchangia Rais wa Tanzania John Magufuli Gharama ya Kuchukua Fomu ya Urais ya mwaka 2020 ili aendelee kutetea nafasi yake ya Urais kupitia chama hicho.
Wameeleza hayo wakati wa ziara ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)Dkt. Bashiru Ally akiendelea na ziara yake Mkoani Mtwara kuelekea jimbo la Ndanda kupitia jimbo la Mtama,
Akieleza kwa niaba ya wazee hao, Mbunge wa jimbo la Mtama Ndg. Nape Mosses Nnaye, ameleeza kuwa wazee wapo tayari na wamejipanga kumchangia gharama za fomu za Urais ili kuonesha mapenzi yao kwake kutokana na namna anavyowajali wazee na wananchi kwa ujumla, hivyo wanasubiri kibali kwa Katibu Mkuu.
Wameyasema hayo asubuhi ya leo tarehe 22 Februari, 2020 katika ufunguzi wa shina la Wakereketwa la Kambarage jimboni Mtama.
Katibu Mkuu pamoja na mambo mengine, akifafanua uamuzi huo wa wazee, ameeleza kuwa, nia yao ni njema na imekuwa matamanio ya wazee wengi kufanya hivyo kama wao wa Mtama, amepokea nia yao njema lakini kikubwa wao waendelee kumuombea Mhe. Rais afya njema ili awatumikie zaidi bila kuchoka.
Katibu Mkuu yupo Mkoani Mtwara kwa ziara ya kikazi ya siku tatu, yenye lengo la kuendelea kukirejesha Chama kwa wanachama.