Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 1:43 pm

NEWS: WAZAIRI AKIRI MATUKIO YA UTESAJI WAPINZANI YANAULIZWA KIMATAIFA

Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Agustino Mahiga, amekiri kuwepo kwa matukio ya utesaji wapinzani na uwepo wa uvunjifu wa amani hapa nchini, huku akisema kuwa matukio hayo ni miongoni mwa maswala yanayoulizwa sana na wananchi na Jumuiya za Kimataifa na serikali inaendelea kuyafuatilia.

Waziri Mahiga amesema matukio hayo yanajulikana Serekalini na vyombo vya Usalama vinafuatilia kwa karibu na Majibu ya upelelezi yanaridhisha.

"kuhusu matukio ya utesaji wa wapinzani na uvunjaji wa haki za binadamu, matukio yanajulikana serikalini na vyombo vya usalama vinafuatilia." amesema Waziri Mahiga

Waziri Mahiga ametoa kauli hiyo Bungeni jijini Dodoma katika muendelezo wa vikao vya Bunge baada ya kuulizwa swali na Mbunge wa CUF Ali Saleh, ambaye alihoji juu ya uwepo wa matukio hayo na kueleza ni uvunjaji wa haki za binadamu.

"Mara nyingi tunapata taarifa na majibu yanaridhisha, kazi ya upelelezi inaweza kuchukua muda, maswali haya yanaulizwa na wananchi, yanaulizwa kimataifa, tupo tayari kutoa taarifa sahihi uchunguzi ukikamilika" ameongeza Mahiga.

Hapa nchini kumekuwepo kwa matukio kadhaa ya Utekaji na Utesajwa wa viongozi na wanachama wa upinzani pamoja na waandishi wa habari kwa siku za hivi karibuni .

Hivi karibuni Mwishoni mwa mwezi huu Kada na mwanachama wa Chadema Mdude Nyangali alitekwa na watu wasiojulikana na kupataikana siku tatu baadae akiwa kwenye hali mbaya, hali amabayo inayoonesha alikuwa na maumivu makali kulingana na kipigo alichokipata kutoka kwa watu hao.

Mimi nilitekwa sikupotea, lile eneo nimeishi kwa miaka 20 siwezi kupotea".

"Ninathibitisha kuwa tukio lililonitokea ni la kisiasa sio la Kijambazi maana maisha yangu ni chini ya dola 100 kwa mwezi" Mdude alieleza waandishi wa habari tarehe 20 mei 2019 baada ya kuapatikana kwake.

Aliongeza kusema kuwa analihusisha na siasa kwa sababu waliomshabulia na waling'ang'ania nyaraka za chama pamoja na za mahakamani wakati wa tukio hilo.

"Kwanini waliniambia niite Umoja wa Ulaya waje wanisaidie, kwanini waliniambie nimwambie Mbowe na Lissu waje wanisaidie?"

Mdude

Kamishina msaidizi wa Polisi, David Misime alisema Mdude alifika katika kituo cha polisi na kuandika maelezo ambayo aliona yanaweza kusaidia jeshi la polisi kufanya uchunguzi, hivyo walichukua taarifa na kufungua jalada la kesi yake huku wakiendelea kufanya uchunguzi na watakapokamilisha uchunguzi huo watatoa taarifa.

"Tunafanya kazi yetu kitaalamu kwa mujibu wa maelezo aliyotoa na tunafanyia kazi na ukweli utabainika na kama kuna hatua za kuchukuliwa zitachukuliwa" Kamishina Misime alisisitiza.