- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WAWILI KORTINI KWA KUANZISHA SACCOS YA MKE WA RAIS MAGUFULI
Dar es salaam. Watu wawili wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es salaam wakikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi mara baada ya kudaiwa kutumia Jina la Mke wa Rais wa Tanzania John Magufuli Bi Janeth Magufuli Kujipatia fedha kinyume na Sheria.
Watuhumiwa hao ni Masse Uledi (43) ambaye ni Mkazi wa Kitunda Magore na Mwingine ni Nkinda Shekalage (34), mfanyabiashara anayeishi Tegeta wazo
Washtakiwa hao wamesomewa mashtaka matatu leo Aprili 16, 2020, mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Augustina Mmbando ambayo ni kuchapisha taarifa za uongo kwenye mtandao, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na kutakatisha fedha.
Katika hati ya mashtaka iliyosomwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Mkunde Mshanga akisaidiana na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon imeeleza katika shtaka la kwanza kuwa kati ya Januari 20 na Machi 31 mwaka 2020 jijini Dar es Salaam na katika maeneo mengine ya ndani ya Tanzania washtakiwa hao kupitia mtandao wa Facebook walichapisha taarifa za uongo.
Imedaiwa walichapisha ujumbe unaosema JANET MAGUFULI saccos "mpya mpya isome tafadhali mkopo yote ni online tuu! na utapata ndani ya dakika 45 tu, mikopo huanzia kutolewa kuanzia laki tatu hadi milioni ishirini kufuata utaratibu huu ili kupata mkopo ..... tuna namba za kitambulisho chako cha mpiga kura au NIDA na majina yako matatu kupitia namba 0685012921 kisha. Piga namba hiyo ili upatiwe namba ya mhasibu ili kuweka akiwa hatimae kupata mkopo...", ambapo walifanya hivyo huku wakijua kuwa si kweli na walikuwa na lengo la kuipotosha jamii.
Katika shtaka la pili imedaiwa, siku na mahali hapo washtakiwa hao kwa njia ya udanganyifu walijipatia Sh. 15,068 650 kupitia muamala wa simu iliyosajiliwa kwa jina la Adam Mamba huku akijua kuwa si kweli.
Aidha, katika shtaka la tatu la kutakatisha fedha imedaiwa washtakiwa hao walijipatia kiasi hicho cha fedha huku wakijua kuwa fedha hizo ni zao la kosa la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.
Hata hivyo, washtakiwa hawakuruhusiwa kujibu chochote mahakamani hapo kwa kuwa kesi wanayoshtakiwa nayo haina dhamana. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Aprili 30 mwaka huu na washtakiwa wote wamerudishwa rumande.