- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WAUMINI,VIONGOZI WA DINI YA KIISLAMU WAPEWA SOMO
Dodoma: WAUMINI wa Dini ya kiislamu pamoja na viongozi wa dini hiyo wametakiwa kujitika zaidi katika kushughulikia masuala ya Kiriho na kimaendeleo.
Wasaa huo ulitolewa jana na sheikh wa Mkuu wa mkoa wa Dodoma Mustafa Shabani alipokuwa akizungumza na wahumini na viongozi wa msikiti wa Mbabala katika manispaa ya Dodoma.
Mkuu huyo wa kiimani amesema umefika sasa waumini wa dini ya kiislamu kutambua kuwa ni wajibu na haki yao kupata elimu ya kawaida na elimu ya kimungu.
Mbali na hilo alisema kutokana na Dodoma kuwa makao makuu ya serikali kuna kila sababu ya muanzisha miradi mbalimbali ambayo itawaingizia kipato na kujishughulisha katika kufanya kazi badala ya kusubiri au misaada kutoka kwa wafadhili.
Sheik Mstaafa akizungumza na wahumini pamoja na viongozi wa msikitu wa Manyema amesema hakuna sababu yoyote ya viongozi wa misikiti pamoja na waumini kutumia muda mwingi kutengeneza migogoro badala yake wanatakiwa kuchangamkia fursa walizonazo.
Amesema msikitu huo ambao kwa sasa unatumika kama nyumba ya ibada ni juhudi za mzee Ujiji ambaye kwa sasa ameisha tangulila mbele ya haki lakini kwa kutambua umuhimu wa himani alijitolea mali zake kujenga nyumba ya Ibada.
Kutokana na hali hiyo aliwataka viongozi wa Dini ya Kiislama pamoja na wahumini kuhakikisha wanabuni miradi mbalimbali ambayo itaweza kuwaongezea kipato sambamba na kwalipa baadhi ya watumishi wa msikitu huo kwa maana ya walimu wa Dadrasa.
Katika hatua nyingine alisema ili uislamu uweze kusonga mbele na kwa kasi kuna haja ya kufikiria kujenga vituo mbalimbali vya huduma kama vile shule,zahanati au vituo vya afya.
Baadhi ya viongozi wa msikiti wa Manyema walimueleza sheikh wa mkoa kuwa wanakabiliwa na changamoto mbalimbali.
Wamezitaja changamoto huzo kuwa ni pamoja na msikitu kukosa umeme.kukosekana vyoo pamoja, sipaka kwa ajili ya mawaidha pamoja na vifaa mbalimbali.
Hata hivyo walimuomba kiongozi wao ifikapo mwezi mtukufu wa Ramadhani waweze kupatiwa ushirikiano hata kwa kutapiwa tende kwa ajili ya kupata ftari pamoja na kukosekana kwa kipato kwa ajili ya kumlipa mwalimu wa Madrasa.
Hata hivyo kiongozi huyp alikubaliani na changamoto hizo na kuhaidi kuwa atazipatia ufumbuzi huku akiwahimiza kuhakikisha wanafanya kazi kwa malengo ya kujiongezea kipato.