Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 7:37 pm

NEWS: WAUMINI WA DINI YA KIISLAMU WATAKIWA KUUTUMIA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI KAMA SEMINA YA KULITAFAKARI NENO LA MUNGU

DODOMA: WAUMINI wa dini ya Kiislamu nchini wametakiwa kuutumia mwezi mtukufu wa Ramadhani kama sehemu ya semina elekezi ya kulitafakari neno la Mungu.

Kauli hiyoimetolewa na sheikh wa Mkoa wa Dodoma Mstafa Shabani Rajabu alipokuwa akitoa mawaidha katika msikiti wa Gadaffi uliopo mjini hapa.

Katika mwaidha hayo amesema waumini wa dini ya kiislamu wanatakiwa kuutumia mwezi mtukufu katika kumwishia maora wao kwa kutafakari matendo mema ambayo Mtume Mohammadi aliyatenda katika kuitafuta haera.

Aidha amesema kwa kipindi cha mwezi mtukufu waumini wa dini ya kiislamu wanatakiwa kuhakikisha wanahudhuria ibada na kupata nafasi kubwa ya kupata mawaidha ya meno la mungu ili kujiwekea kipimo cha kujitadhimini juu ya uchaji wa Mungu wao.

Mbali na kuudhuria ibada Sheiki Msitafa amesema kipindi cha mfungo wa mwezi mtukufu wa ramadhani ni kipindi cha kuomba toba na rehema za Mungu ikiwa ni pamoja na kutoa misamaha kwa watu ambao wamekoseana na si vinginevyo.

Pia amewaelekeza waumini wa dini hiyo kuhakikisha wanatoa sadaka kwa watu wenye uhitaji, kama vile makundi ya watoto yatima,wazee, wajane na wale wote ambao wanauhitaji kadri ya mtoaji atakavyojaliwa na Mwenyezi Mungu.

“Kwa kipindi hiki ni kipindi ambacho ni cha kutafuta rehema za Mwenyezi Mungu, lakini ni kipindi cha kuwasaidia watu wenye uhitaji kwa kufanya hivyo ni wazi kuwa Mwenyezi Mungu anatoa dhawtu hata kama utaweza kumfuturisha mtu tende moja kadri utakavyojaliwa ndivyo Mungu atakavyokuhesabia dhawabu” alisisitiza sheik wa Mkoa.

Pamoja na mambo mengine amewakemea waislamu ambao wmekuwa ni waislamu wa Ramadhani ambao kipindi cha mwezi mtukufu ukiisha wanaanza kujiingiza katika anasa za kila aina na kusahau kuwa wanatakiwa kuendelea kumcha Mwenyezi Mkungu na kuenzi Matendo mema ya Mtume.

“Wapo baadhi ya waumini wa dini ya kiislamu ambao ni waislamu wa Ramadhani,wamafungu lakini pale mwezi Mtukufu ukiisha wanajichanganya katika matendo maovu ya kunywa pombe, uzinzi na biashara haramu kama vile madawa ya kulevya ma mambo mengine ambayo hayampendezi Mungu.

“Kipindi hiki ni cha kujitafakari na pale mfungu unapoisha unatakiwa kujitafakari na kuona umefanikiwa wapi Kiroho, au umechelewa wapi ili uweze kujitafakari kwa kuendelea na uchaji wa kumtafuta Mungu ili uweze kupata rehema na mwishowe uipate pepo kama ilivyo ahadi ya Mtume” alisisitiza Sheiki wa Mkoa.

Katika hatua nyingine aliwasii wafanya biashara kujiepusha na tama ya kupandisha vyakula wakati wa kipindi hiki cha mfungo mtukufu wa Ramadhani na kueleza kuwa kwa kufanya hivyo ni kumchukiza Mwenyezi Mungu.

Amesema kwa ujumla kama wafanyabiashara watakuwa na tama ya kupandisha bei ya vyakula kwa kipindi cha Mwezi Mtukufu ni wazi watakuwa wanatafuta faida ya duniani lakini kwa Mungu hawawezi kupata Dhawabu kwani kwa kufanya hivyo ni sawa na kuwakomoa waumini wa dini hiyo ambao kwa sasa wapo katika mwezi wa toba na kujitafakari.