- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WAUGUZI WAWILI WATIWA MBARONI KISA ELF 10
GEITA: Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoani Geita imewaburuta mahakamani watumishi wawili wa Hospitali ya Wilaya ya Bukombe wakikabiliwa na mashtaka mawili tofauti likiwemo la kuomba na kupokea rushwa.
Walioburuzwa mahakamani ni Elizabeth Emanuel ambaye ni muuguzi na David Zakayo ambaye ni mhudumu wa afya katika hospitali hiyo.
Mwendesha mashtaka wa Takukuru mkoani geita, Kelvin Murusuri ameieleza mahakama kuwa washtakiwa wote kwa pamoja waliomba na kupokea rushwa ya Sh10, 000.
Wakisomewa mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi, Veronica Selemani, washtakiwa hao wamedaiwa kutendo kosa hilo Julai 13, kinyume na kifungu cha 15 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa namba 11 ya mwaka 2007.
Katika maelezo ya makossa hayo ilielezwa kuwa wakiwa eneo lao la kazi, washtakiwa hao kwa pamoja wanadaiwa kuomba kiasi hicho cha fedha kutoka kwa mgonjwa aliyeelezwa kuwa ni mzee mwenye umri wa miaka 72 ambaye hata hivyo hakutajwa jina.
Fedha hizo zilidaiwa kuwa ni gharama za mzee huyo kupatiwa majibu ya vipimo alivyochukuliwa alipofika hospitalini hapo kwa matibabu.
Kwa mujibu wa Sera ya Taifa ya Wazee ya Mwaka 2003, mgonjwa huyo hakutakiwa kulipia gharama za matibabu.
Washitakiwa wamekana mashitaka na kuachiwa kwa dhamana ya hati ya mali isiyohamishika yenye thamani ya Sh4 milioni na wadhamini wawili hadi Agosti 16, shauri hilo litakapokuja kwa ajili ya kusomewa maelezo ya mashtaka baada ya upande wa Jamhuri kueleza kuwa upelelezi umekamilika.