- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WAUGUZI FANYENI KAZI KWA PAMOJA.
DODOMA:Wauguzi wote nchini wametakiwa kufanya kazi kwa pamoja na kuacha tabia za ubinafsi ili kuweza kuwasaidia wananchi wanaofika kwenye vituo vya kutolea huduma za afya kupata huduma bora na kwa wakati.
Hayo yamesemwa na katibu mkuu Wizara ya afya Dkt. Zainab Chaula aliposhiriki kikao cha kuwashirikisha wadau mwongozo wa utoaji huduma kwa kuzingatia utu,heshima na maadili kilichofanyika jijini hapa.
Dkt. Chaula alisema kuwa taaluma ya uuguzi ni ya wito hivyo wanatakiwa kuzingatia weledi wa fani yao ili kuwa na mafanikio ya utoaji huduma za afya nchini ili kuokoa maisha ya watanzania ambao wanahitaji msaada wa kuokoa kutoka kwa wataalam hao.
“Lazima turudishane kwenye mstari ili tuweze kuokoa maisha ya akina mama wajawazito,watoto na wagonjwa wengine ,tujiulize kwanini akina mama wajawazito wanafariki?nyinyi ndio chachu ya mabadiliko katika utoaji wa huduma”.Alisisitiza Dkt.Chaula.
Aidha, katibu mkuu huyo alisema kuwa katika kutimiza wajibu wa wauguzi kwenye vituo vya kutolea huduma za afya anatamani kusiwepo na kifo hata kimoja hususani upande wa akina mama wajawazito hivyo inahitajika nguvu ya pamoja na uelewa miongozi mwa wauguzi kote nchini ili ifikapo 2020.
Mkakati wa kitaifa wa kupunguza vifo wa vitokanavyo na uzazi tanzania imekusudia ifikapo mwaka 2020 kupunguza vifo hivyo kufikia 292 katika vizazi hai laki moja ukilinganisha na mwaka 2015 vya vifo 556 kwa vizazi hai laki moja.