- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WATUMSHI HEWA 9,932 WATUMBULIWA BAADA YA JPM KUKABIDHIWA RIPOTI YA UHAKIKI WA VYETI KWA WATUMISHI WA UMMA.
Dodoma: RAIS. Dkt John Pombe Magufuli amewatumbua watumishi hewa 9,932 na kuwafuta kazi kuanzia leo watumishi hao baada ya kubainika wamefoji vyeti vyao vya elimu yao.
Pamoja na hivyo amesema wale wote watakaokaidi amri hiyo hadi kufikia Juni 15 wakamatwe na wapalekwe mahakamani.
Magufuli ametoa kauli hiyo katika ukumbi wa chimwaga udom mjini hapa kwenye upokeaji wa taarifa za uhakiki wa watumishi na uzinduzi wa miaka 10 ya Chuo Kikuu cha Dodoma.
Katika zoezi hilo jumla ya watumishi 435,000 wa umma nchini walifanyiwa uhakiki ambao huo.
Amesema watumishi hao ambao wamefutwa kazi majina yao yachapishwe kwenye magazeti ili wote wajulikane.
“ Nasema hawa wachapishwe kwenye magazeti ili hata kama kuna baba yako alikuwa anatumia cheti feki ajulikane,
‘’ Hawa ni majambazi na majizi kama majizi wengine hakuna sababu ya kughushi vyeti ndiyo upate ajira nenda kwenye ajira inayoendana na ngazi ya cheti chako kwani makuli kule bandarini wanahitaji digrii ni mabega tu’’ amesema.
Amesema watumishi wengine 1,538 ambao vyeti vyao vina utata kwa kutumiwa na watumishi zaidi ya mmoja lakini amesema watumishi hao wachunguzwe kwa kina na kujua ni cheti cha nani.Rais amesema vyeti hivyo vinatumika na watumishi 3,076 ambao wamekuwa wakitumia jina moja au kuongeza majina katika vyeti hivyo.
“ Hawa nao wakisha chunguzwa ijulikane ni cha nani na huyo ndiye ataanza kupewa mshahara na si vinginevyo’’ alisema.
Kwa mujibu wa Rais amesema wanaosababisha kuwepo kwa watumishi hewa ni viongozi na mara nyingine hata wanasiasa wapo.
“Hata mimi nilipokuwa shuleni nilikuwa nawachukia sana wanasiasa wanasema jambo halafu hawatekelezi bahati mbaya sasa ameingia rais ambaye si mwanasiasa hapa ni kazi tu,
‘’Hivi hawa watumishi hewa walikuwa wametoka wapi kwani kulikuwa hakuna mawaziri, makatibu mkuu, ingawa hatupo hapa kumsema mtu lakini ni vizuri kukumbuka hata dahambi zao ili kujirekebisha’’ amesemaAmesema kulikuwa na watumishi hewa 19,706 ambapo serikali ilikuwa ikitumia bilioni 238 kwa mwaka kama mishahara.
Awali akitoa maelezo ya kazi hiyo ya uhakiki Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi wa umma na Tawala Bora Angela Kairuki amesema uhakiki huo ulifanyika katika maeneo mbalimbali ikiwemo vyeti halali,vyeti vilivyofoji na vyeti vyenye utata.
Amesema zoezi hilo ni endelevu kwani serikali haiwezi kuwa watalaam ambao hawana sifa kwani wanalikosesha taifa fedha nyingi wakati hawana sifa.
Ambapo Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam,ambaye anatuhumiwa kutumia vyeti feki anenusurika kuondolewa katika nafasi yake baada ya Waziri wa Nchi,ofisi ya Rais Menejimenti ya utumishi wa Umma na Utawala Bora,Angella Kairuki kutangaza kuwa ripoti ya ukaguzi wav yeti feki hauwahusu watumishi wa kisiasa ambao ni wakuu wa mikoa, wakuu wa Wilaya na pamoja na Mawaziri.