- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WATUMISHI WOTE WA MIFUKO YA HIFADHI KUCHUKUA MAFAO YAO
Wafanyakazi wa umma na wasekta binafsi nchini Tanzania ambao walikuwa wakiweka fedha zao kwenye Mifuko ya Hifadhi ya Jamii , sasa wako uhuru kisheria wa kudai mafao yao muda wowote waliotumikia kazini.
Hatua hiyo inatokana na wanufaika hao kuondolewa vikwazo vya muda wa kudai mafao yao, baada ya Bunge kupitisha Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali Namba Sita wa mwaka 2019.
Kwa maana hiyo, wanufaika hao watakuwa huru kudai mafao yao muda wowote wanaohitaji kufanya hivyo kulingana na utayari wao.
Muswada huo uliwasilishwa Bungeni na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Profesa Adelardus Kilangi Septemba 12,mwaka huu ambapo wabunge waliridhia mabadiliko ya vifungu katika Sheria ya Mamlaka ya Udhibiti wa Hifadhi za Jamii Sura ya 135, iliyotungwa na Bunge mwaka 2008