- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WATUMISHI WA SEREKALI WAPIGWA MARUFUKU KUDAI NYONGEZA YA MSHAHARA
Serikali kupitia Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi na utawala bora) Dk. Mary Mwanjelwa imesema watumishi wa umma wote hawapaswi kuomba nyongeza ya mwaka ya mshahara, bali Serikali yenyewe ndiyo yenye uwamuzi wa kutoa au kutotoa nyongeza hiyo.
Kauli hiyo ya Dk Merry ameitoa leo bungeni leo Mei 14, wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Tunza Issa Malapo wa Chadema.
Malapo alitaka kujua serikali inatumia sheria ipi kutowapa wafanyakazi stahiki zao zinazohusu kupandishwa madaraja, na ongezeko la mwaka.
Katika majibu yake, Dk. Mwanjelwa amesema kwa mujibu wa kanuni E.9 (1) ya kanuni ya kudumu katika utumishi wa umma za mwaka 2009, toleo la tatu, nyongeza ya mwaka ya mishahara haipaswi kuombwa.
Siku ya May mosi ya mwaka huu Mkoani Mbeya katika ziara yake Rais Magufuli aliwataka wafanyakazi kuwa na subira katika ombi lao la kuongezewa mishahara na akaahidi kuwaongezea mishahara hiyo kabla hajamaliza kipindi chake cha uongozi.
“Nawasihi ndugu wafanyakazi kuendelea kuchapa kazi kwa bidii ili kuiletea maendeleo nchi yetu, Wazee wetu wa zamani walijitoa mhanga kuikomboa nchi yetu kisiasa, ni jukumu letu kizazi cha sasa kujitoa mhanga kuikomboa nchi yetu kiuchumi” alisema Mhe. Rais Magufuli.
Rais Magufuli alisema baada ya uhakiki kufanyika Serikali imetoa nyongeza ya mshahara ya shilingi Bilioni 72.8 kwa wafanyakazi 505,985, imelipa malimbikizo ya mishahara ya shilingi Bilioni 75.5 kwa wafanyakazi 50,386, imelipa shilingi Bilioni 29.5 kwa wafanyakazi 118,989 waliopandishwa madaraja, imelipa shilingi Bilioni 291.3 kwa madai ya wafanyakazi yasiyo ya mshahara na kwamba wafanyakazi wengine 193,166 watapandishwa madaraja mwaka ujao wa fedha.