Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 12:24 am

NEWS: WATUMISHI 3 IDARA YA AFYA MBARONI KWA KUUZA DAWA ZA SEREKALI

GEITA: Watumishi watatu wa idara ya afya wa Zahanati ya Mutundu Wilayani Chato mkoani Geita, wamefikishwa mahakamani na Jeshi la polisi Mkoani humo kwa tuhuma za kuuza dawa za serikali zaidi ya Maboksi 150.

Related image

Akizungumza na Waandishi wa habiri Leo Jumanne Machi 12, 2019 Kamanda wa Polisi mkoani Geita Mponjoli Mwabulambo wamewakamata watuhumiwa wawili mmoja ni Balamiliusi kamugisha aliyekamatwa eneo la Buselese wilayani Chato, ambapo alikamatwa akiwa na dawa mbalimbali mali ya serekali, ambapo alikamatwa na boksi 36 za madawa aina ya Aluu 1*6, na Aluu1*24 boksi 15, MRDT 39, Carvits Kopo 2, Cypris kopo 1, na vifaa vingine vya kitabibu

" hizi dawa zinadhaniwa kuwa ni mali ya serekali na ninapo zungumza sasa watuhumiwa wote watatu wemeshafikishwa mahakamani, kwahiyo ukiangalia mahusiano ya kukamatwa kwao, wanaonekana wanafani za kitabibu" amesema Kamanda Mwabulambo