Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 3:31 am

NEWS: WATUHUMIWA MAUWAJI YA WATOTO NJOMBE WABURUZWA MAHAKANI LEO

Njombe: Watuhumiwa watatu wa utekaji na mauaji ya watoto wilayani Njombe wamefikishwa katika Mahakama ya Hakim Hakimu mkazi Njombe leo Jumanne Februari 12, 2019.

Watuhumiwa hao ni Joel Nziku ambaye ni mtuhumiwa wa mauaji ya watoto watatu wa familia moja , Mwingine ni Danford Nziku mkazi wa Ikando halmashauri ya wilaya ya Njombe, Nasson Kaduma, na Alphonce Danda.

Hii ni mara ya kwanza kwa watuhumiwa wa mauwaji hayo kufikishwa mbele ya mahakama tangu kutokea kwa mauwaji hayo.

Inaarifiwa kuwa mpaka sasa jumla ya watoto 29 wameuwawa kikatili katika sakata hilo huku watu wengi wakihusisha matukio hayo na imani ya Kishirikina

Nje ya mahakama hiyo ulinzi umeimarishwa kutokana na polisi kusambaa kila kona, huku msafara wa watuhumiwa hao ukisindikizwa na magari sita ya polisi.

Juzi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama nchini Generali Venance Mabeyo aliwasili mjini njombe ili kuongezea nguvu juu ya janga hilo liloikumba Tanzania