- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WATU ZAIDI YA 160 WAMEUWAWA KWENYE MILIPUKO YA MABOMU SRI LANKA
Watu zaidi ya 160 wameuawa kutokana na mfululizo wa mabomu yaliyoripuka kwenye mji mkuu wa Sri Lanka, Colombo. Polisi imethibitisha kuwa watu wengine zaidi ya 300 wamejeruhiwa.
Kwa mujibu wa msemaji wa polisi Ruwan Gunasekera mlipuko mwingine umetokea muda mfupi katika hoteli iliyopo jimbo la kusini mwa Colombo la Dehiwala likiwa ni shambulio la saba kufanyika katika siku hii ya Jumapili. Mlipuko wa nane umetokea kwenye kitongoji cha Orugodawatta kaskazini mwa mji mkuu.
Mpaka sasa hakuna yeyote aliyedai kuhusika na mashambulio hayo na wala idara za usalama hazijasema iwapao mashambulo hayo yalifanywa na magaidi.
Lakini kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya habari mashambulio hayo yalizilenga sehemu za kidini na kiuchumi. Rais wa Sri Lanka Maithripala Sirisena amesema majeshi ya ulinzi na polisi wameanzisha uchunguzi. Viongozi mbalimbali duniani wamelaaani mashambulio hayo.