- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WATU WENYE UALBINO WALIA NA SHERIA YA MTANDAO
DODOMA: CHAMA cha watu wenye ualbino nchini,kimeitaka serikali kuhakikisha inafuatalia kwa ukaribu matukio mbalimbali ambayo wanakutananayo na kuyapati uzito kama ilivyo kwa Faru John.
Akizungumza na waandishi wa habari Mwenyekiti wa Chama cha maalbino COLMAN TEMBA,amesema licha ya serikali kuonesha juhudi za kupambana na ukatili kwa watu wenye ualbino lakini bado kuna mapungufu makubwa.
Amesema kwa sasa serikali imepitisha sheria ya makosa ya mtandao bado sheria hizo zimekuwa zikiwalenga watu ambao wanaonekana kuwa na nafasi kubwa serikalini lakini siyo katika jamii ya watu wenye ualbino.
Akitoa ufafanuzi zaidi Colman amesema hivi karibuni,kulitokea kauli za kuudhi kwa msemaji wa timu ya Simba, Haji Manalla alitukanwa kwa njia ya mitandao lakini hakuna hatua yoyote ambayo ilitolewa.
“Tumekuwa tukishuhudia inapotokea mambo ya kuwakashifu viongozi wa serikali katika mitandao wanachukuliwa hatua haraka sana, pia tumekuwa tukishuhudia hatua mbalimbali zinazochukuliwa kwa baadhi ya wanyama mfano Faru John.
“Lakini inapotokea matukio yanayowagusa watu wenye ualbino japo hatua zinachukuliwa lakini haziwi za haraka na kali kama inavyotendeka katika makundi mengine” amesema Temba.
Katika hatua nyingine Temba amesema Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu,sera Bunge,Ajira,Vijana na Watu wenye Ulemavu,Jenista Mhagama anatarajiwa kuwa ngeni rasmi katika Maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya uelewa juu ya wayu wenye ualbino mjini Dodoma.
Amesema maadhinisho hayo yanalenga kutoa elimu kwa jamii ili kuhakikisha wanatambua umuhimu wa kuwepo au kushirikiana na watu wenye ulemavu.
Amesema katika maadhimisho hayo kauli mbuiu itakuwa “Takwimu na Tafiti kwa ustawi wa watu wenye Ualbino”.
Amesema jamii inatakiwa kutambua kuwa watu wenye ualbino wanatakiwa kupata haki sawa kama watu wengine ikiwa ni pamoja na kupatiwa elimu pamoja na kutoa ajira kwa mtu mwenye sifa.
Mbali na hilo aliwataka watu wenye ualbino kujitambua na kujiamini na kuachana na tabia ya kujinyanyapaa na badala yake wajitambue na kudai haki zao ikiwa ni pamoja na kuhamasisha elimu kwa watu wenye ualbino.