November 26, 2024, 11:12 pm
- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WATU WAWILI WAFARIKI DUNIA KWA KUCHOMWA MOTO.
Kauli hiyo imetolewa jana mjini hapa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora Wilbrod Mutafungwa wakati wa mkutano na waandishi wa habari.
Alisema kuwa hatua hiyo ilitokana na watu hao ambao hadi hivi sasa majina yao hajajulikani kumukodisha na kisha kumteka dereva bodaboda na walipofika eneo la Malolo lililopo Manispaa ya Tabora walianza kumchoma kisu kwenye shavu la kushoto kwa nia ya kutaka kumpora pikipiki.
Mutafungwa alisema kuwa baada ya Dereva wa Bodaboda kuchomwa kisu alipiga kelele za kuomba msaada na wananchi walijitokeza , baada ya wezi kuona watu wanakuja walijaribu kukimbia lakini hawakufanikiwa kufika mbali na ndipo walikamatwa na kuanza kupigwa hadi walipofariki.
Alitoa wito kwa watu ambao ndugu zao hawaonekani kufika Hospitali ya Mkoa wa Tabora Kitete kuwatambua watu hao ambao majina hayo haya fahamiki.
Kamanda Mutafungwa alisema kuwa Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo ili kubaini majina ya watu hao na watu ambao wamekuwa wakishiriana nao katika vitendo vya kihalifu ikiwemo utekaji wa Boda boda.
Aliongeza kuwa wanaendelea na uchunguzi wa watu waliohusika katika kujichukulia Sheria mkononi ili waweze kufikishwa katika vyombo vya maamuzi.
Naye Mwenyekiti wa Chama cha Waendesha Bodaboda Manispaa ya Tabora Waziri Kipuzi aliwataka madereva kuwa makini na watu wanawakodisha nyakati za usiku kwani wapo ambao wana nia mbaya.
Katika hatua nyingine Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora Wilbroard Mtafungwa alisema kuwa hadi hivi Jeshi hilo linawashikilia watu 54 kwa tuhuma za kuhusika na tukio la kuwapiga na kuwachoma moto katika sehemu zao za siri wanawake wanne katika kata ya Loya wilaya ya Uyui.