- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WATU 7 WASHIKILIWA NA POLISI KWA KUPANDISHA BEI YA SUKARI
Serekali imewatia mbaroni wafanyabiashara saba mkoani Tanga kwa kujihusisha na kuuza sukari kwa bei ya juu zaidi ya ile iliyopangwa na Serikali kama bei elekezi mwishoni mwa wiki hii.
Afisa Miliki Mwandamizi wa Bodi ya Sukari, Mhandisi Ali Mwinyimanga alisema Serikali haitavumilia wafanyabiashara yoyote ambaye anaongeza bei kwa lengo la kuwaumiza wananchi,wakati tayari nchi inasukari ya kutosha.
“Hili ongezeko la sukari, ni la kutengeneza tuu,tulichogundua wafanyabiashara wametumia janga la vorona kueleza sukari imeadimika jambo ambalo halina ukweli,”alisema.
Mwinyimanga alisema kazi ya kuwatafuta wafanyabiashara walanguzi ,ni endelevu mpaka pale wafanyabiashara watakapoweza kuuza kwa bei elekezi iliyowekwa na serikali.
“Tunachotaka ni kuhakikisha kuanzia mkulima ,mzalishaji hadi mtu wa mwisho ambaye ni mlaji anapata haki yake bila ya kumnyonya kama kule inapozalishwa bei haijapanda iweze wewe muuzaji ndio upandishe bei,”alisema.
Alisema ukaguzi huo, ni endelevu mpaka pale bodi ya sukari itakapojiridhisha kuwa sukari inauzwa kwa mujibu wa maelekezo yaliyotolewa na serikali.
Ofisa Mwandamizi Uchunguzi wa Tume ya Ushindani (FCC), David Mawi alisema tume ilipata malalamiko ya walaji kuhusu kuadimika kwa bidhaa hiyo pamoja na bei kubwa.
Alisema tume, imeamua kufanya uchunguzi ili kujiridhisha na malalamiko hayo kama yana ukweli kiasi gani.
“Tunachunguza kujiridhisha kama uhaba huo sio wa kutengeneza na washindani wa soko au kupangwa na washindani katika soko,” alisema.
Alisema baada ya kupata taarifa za kutosha kuhusu kero hiyo, watazifanyia kazi na kujana majibu ambayo yataweza kuwa suluhisho kwa wananchi ambao ni walaji wa mwisho