- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WATU 6 WAUWAWA KWA KUPIGWA RISASI MTWARA
Mtwara. Watu sita wameuawa kwa kupigwa risasi na wengine 7 kujeruhiwa katika kijiji cha Ngongo Wilaya ya Tandahimba mkoani Mtwara katika mpaka wa Tanzania na Msumbiji baada ya kuvamiwa na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia Jumanne Novemba 12, 2019.
Kwamujibu wa Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Boaz amesema Watanzania sita walipigwa risasi na watu wanaodhaniwa kutoka nchi jirani ya Msumbiji wakati wakiwa visiwa vya mto Ruvuma wanakofanya shughuli za kilimo.
“Usiku walivamiwa na kikundi cha watu waliowakusanya pamoja na kuwapiga risasi. Watu sita walifariki dunia na wengine saba walijeruhiwa na wamelazwa Hospitali ya Tandahimba.”“Jeshi la polisi na vyombo vingine vya dola tutachukua hatua madhubuti kuhakikisha wote waliohusika na tukio hili wanapatikana na kuchukuliwa hatua,” amesema DCI Boaz.
Amewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa vyombo vya dola ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa sahihi na kuwataka wananchi kuchukua tahadhali wanapokwenda nchi nyingine kufanya shughuli za kiuchumi.umi.
Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi, Liberatus Sabas amesema kutokana na kazi nzuri wanayoifanya ndio maana wahalifu wanafanya matukio hayo mipakani.
“Tusikubali hata siku moja wavuke mpaka waje huku ndani tupo bega kwa mbega na wananchi. Vyombo vyote vya ulinzi na usalama vipo pamoja tutawasaka, tutawatia mbaroni na hatua kali zitachukuliwa.”
“Kama alivyosema (Boaz) wengine wako humuhumu ndani tuwafichue pamoja, sisi tunaelekea eneo la tukio lakini tone la damu ya Mtanzania haliwezi kupotea bure,” amesema.