- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WATU 52 WAMENUSURIKA KIFO TANGA
Taarifa kutoka mkoani Tanga ni kwamba Zaidi ya abiria 52 waliokuwa wamepanda basi la kampuni ya Kilimanjaro lililokuwa likifanya safari zake kutoka jijini Arusha kuelekea Dar es Salaam, wamenusurika kifo baada ya basi hilo kuacha njia na kupinduka mara mbili eneo la Mkata, wilayani Handeni, Mkoa wa Tanga.
Kwamujibu wa Kamanda wa Polisi, Mkoani humo, Edward Bukombe, alithibitisha kutokea ajali hiyo na kusema ilitokea jana saa tisa mchana, baada ya basi hilo kuteleza na dereva kushindwa kulimudu.
“Inaonekana basi lilipoteleza, dereva ambaye hadi sasa jina lake halijafahamika kwa sababu ana hali mbaya, alishindwa kulimudu na hivyo kupinduka.
“Pamoja na hayo, waliojeruhiwa ni abiria 18 na sita kati yao, walipata majeraha makubwa na kulazimika kupelekwa kwenye Kituo cha Afya Mkata kwa ajili ya matibabu zaidi.
“Kati ya majeruhi hao, wanawake ni 15 na wanaume ni watatu,” alisema Kamanda Bukombe.