- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WATU 45 WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA MADAWA YA KULEVYA
DODOMA: JESHI la Polisi Mkoani Dodoma linawashikilia watu 45 kwa tuhuma mbalimbali ambapo limefanikiwa kukamata silaha,nyara za serikali ikiwemo mali za wizi pamoja na madawa ya kulevya katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Dodoma.
Kauli hiyo imetolewa leo Mjini Dodoma na Kamishina mwandamizi msaidizi wa Jeshi la Polisi,Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma LAZARO MAMBOSASA wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.
Kamanda MAMBOSASA amesema kuwa kutokana na msako unaoendelea kufanywa na Jeshi hilo la Polisi Mkoani Dodoma wameweza kuwakamata watuhumiwa hao katika matukio tofauti ambapo katika tukio la kwanza lilikuwa Wilayani Chemba katika Kijiji cha Mwaikisabe tarafa ya Goima kwakushirikiana na Idara ya wanyama pori waliweza kumkamata mtuhumiwa BASHIRU KADIRI akiwa na silaha mbili aina ya Gobore za kienyeji pamoja na risasi 12 ambazo anadaiwa kutumia katika uwindaji haramu.
Pia Kamanda MAMBOSASA amesema kuwa katika tukio jingine ambalo ni la tano lilitokea katika Manispaa ya Dodoma walikamatwa jumla ya watuhumiwa 21 ambao ni wavunjaji wanaohifadhi mali za wizi na wanunuzi wa mali za wizi hapa anazitaja mali hizo za wizi.
Katika tukio jingine amesema kuwa mnamo Julai 17 mwaka huu alikamatwa HERISON MKOKA mwenye umri wa miaka 38 mkazi wa Kihonda Morogoro ambaye anadaiwa kuwa ni muhalifu alkiyekuwa akitafutwa kwa muda mrefu kwa makosa ya kuwalewesha wanawake kwa kuwawekea dawa za usingizi aina ya Lorivarin two kwenye vinywaji na kisha kuwabaka.
Kamanda huyo amesema kuwa katika tukio jingine ambalo ni la dawa za kulevya waliweza kuwakamata watuhumiwa 14 wakiwa na Bhangi yenye uzito wa gramu 2601 pamoja na misokoto 2601.
Pia ametoa onyo kwa wale wote ambao wanajihusisha na ualifu kwamba Dodoma sio eneo salama kwao hivyo waache mara moja vitendo hivyo.