Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 4:47 pm

NEWS: WATU 41 WAMETEKETE KWENYE AJALI YA NDEGE YA URUSI

Urusi: Watu 41 wameuawa baada ya ndege ya Urusi kutua kwa dharura na kulipuka moto katika uwanja wa ndege wa Sheremetyevo mjini Moscow.

Baadhi ya abiria walitumia mlango wa dharura na kufanikiwa kutoka kwenye ndege hiyo ya Aeroflot iliyokuwa inateketea moto.

Image result for Sukhoi Superjet-100 crush russia

"Watu 37 wamenusurika kifo kati ya hao Abiria ni 33 na maafisa 4 wa ndege hiyo," amesema afisa wa kamati ya uchunguzi, Yelena Markovskaya.

huku Watu watano wamepelekwa hospitalini bado haijajulikana kama watapona au la.

Aeroflot, shirika la ndege la kitaifa Urusi limesema ndege hiyo ililazimika kurudi katika uwanja wa ndege " kutokana na sababu za kiufundi", lakini halikufafanua zaidi.

Ndege nyingine zimelazimika kuelekezwa katika viwanja vingine wa ndege nchini.

Image result for Sukhoi Superjet-100 crush russia

taarifa zinasema kuwa Ndege hiyo aina ya Sukhoi Superjet-100, iliondoka uwanja wa ndege wa Sheremetyevo kwenye majira ya saa 18:02 kwa saa ya huko kutoka eneo la Murmansk.

Maafisa wa ndege wakatoa tahadhari ya wasiwasi wakati kulishuhudiwa " hitilafu" muda mfupi baada ya ndege kuondoka.

Baada ya kutuwa kwa dharurua katika uwanja huo wa ndege , injini za ndege hiyo ziliwaka moto katika njia kuu wa ndege, Aeroflot limesema katika taarifa.

Maafisa hao wa ndege "walijitahidi kadri ya uwezo wao kuwaokoa abiria ," waliofanikiwa kutolewa katika muda wa sekundi 55, shirika hilo la ndege limeeleza.

Aeroflot limechapisha orodha ya walionusurika mkasa huo (kirusi) ambao kufikia sasa wametambuliwa, likiongeza kwamba litaendelea kutoa taarifa kadri wanavyozipokea.

Taarifa pia zinaashiria kwamba ndege hiyo haikufanikiwa katika jaribio la kwanza la kutuwa kwa dharura.

Kaimu Gavana wa mji eneo hilo la Murmansk, Andrey Chibis inaarifiwa amesema familia za waliofariki katika mkasa huo watalipwa $15,300 kola mmoja, huku waathirikwa watatibiwa katika hospitali na watapewa $7,650 kila mmoja.

Mikhail Savchenko anadai alikuwa ndani ya ndege hiyo wakati ilipolipuka moto lakini alifanikiwa "kuruka nje".

Alituma video ya abiria waliokuwa wakitoroka kutoka kwenye ndege hiyo iliyokuwa inawaka moto na kuandika ujumbe: "'niko sawa, niko hai na salama."

Mojawapo ya manusura, Dmitry Khlebushkin, amesema anawashuru sana wahudumu wa ndege hiyo.

"Shukran sana kwa wahudumu, nimenusurika," amewaambia waandishi habari