- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WATU 28 MBARONI KWA KUWASHAMBULIA POLISI GEITA
Geita: Jeshi la Polisi mkoani Geita linawashilikia watuhumiwa 28 wa kijiji cha Nyijundu kata ya Nyang'hwale kwa tuhuma za kuwashambulia na kuwajeruhi askari wa jeshi la polisi watatu waliokuwa wakimzuia mtuhumiwa wa ujambazi kuuawa hadharani na wananchi.
Wakati askari anawazuia wananchi wasimuue mtuhumiwa huyo, wakiwa na silaha za jadi waliwavamia na kuanza kuwapiga kwa silaha za jadi polisi hao
Akizungumza na waandishi wa habari jana Jumatatu Aprili 1, 2019 kamanda wa polisi mkoani Geita, Mponjoli Mwabulambo amesema askari wake wamejeruhiwa na wananch hao, na kuwataja waliojeruhiwa kuwa ni Omari ambaye ni mkaguzi wa Polisi tarafa ya Nyangwale. Mwingine ni askari H16 D/C Yusuph aliyejeruhiwa mguu wa kulia na H4311 D/C Joseph aliyelazwa chumba cha uangalizi maalumu (ICU) katika Hospitali ya Rufaa Bugando jijini Mwanza.
Akielezea tukio hilo, Mponjoli amesema Jumamosi Machi 30, 2019 kundi la majambazi wakiwa na silaha za jadi walivamia nyumba za wakazi wawili kijiji cha Nyijundu na kumuua mkazi mmoja na kujeruhi wengine watatu kisha kupora fedha.
Amesema kufuatia hali hiyo, wananchi walipiga yowe na kuanza msako kwa kushirikiana na polisi na walipomkamata mmoja waliyedhani ni mtuhumiwa na kumhoji kisha kukiri walitaka kumuua na walipozuiwa na polisi wakawageuzia kibao.