Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 2:43 am

NEWS: WATU 19 WAMEFARIKI DUNIA AJALI YA COSTA KUGONGANA NA LORI MBEYA

Mbozi: Watu 19 wamefariki dunia papo hapo baada ya basi aina ya Toyota Coaster mali ya Kampuni ya Komkia lililokuwa likisafiri kutokea Jijini Mbeya kwenda Tunduma, mkoani Songwe kugongwa kisha kulaliwa na lori lililokuwa likitokea Tunduma kwenda Dar es salaam.

Katika Ajali hiyo wanaume walikuwa 15 na wanawake 4, hakuna mtoto hata aliyekuwepo kwenye AJALI hiyo.

Ajali hiyo ilitokea jana katika eneo la mlima Senjele uliopo wilayani Mbozi kilometa chache kutoka mpakani mwa Mbeya na Songwe, ambapo inadaiwa lori hilo lilishindwa kusimama na kuligonga lori jingine lililokuwa limebeba shehena ya mahindi likitokea mkoani Songwe na kuligonga basi hilo na kisha kulilalia basi hilo lililokuwa na abiria 17 ambao wamekufa wote.

Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Brigedia Jenerali mstaafu, Nicodemus Mwangela aliungana mapema kwenye Ajali hiyo katika kuokoa majeruhi kwenye ajali.

Mwangela alisema alipokea taarifa ya ajali hiyo muda wa saa nne usiku na kufika eneo la tukio mara moja. Alisema ajali hiyo ni moja ya tukio baya kutokea mkoani humu tangu Januari mwaka huu. Aidha amewapongeza wananchi na askari wa Jeshi la Polisi waliofika usiku huo ili kuokoa majeruhi na kuweka hali ya utulivu ili kuruhusu njia kupitika na watumiaji wengine.

Miili yao imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya Mkoa wa Songwe na miili mingine miwili imehifadhiwa katika hospitali ya Ifisi katika mji mdogo wa Mbalizi.

“Miili ya abiria hao ambao imekatikakatika vipande vipande isipokuwa watu wawili ambao ni mwanamke na mwanaume ambaye ni dereva wa lori aliyekuwa na mwanamke huyo, wote hawajatambulika walikimbizwa katika Hospitali ya IFISI Jijini Mbeya walikufa muda mfupi wakati wakipatiwa matibabu na kufikisha vifo 19,” amesema Dk Kagya.