Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 2:47 am

NEWS: WATU 17 MBARONI KWA WIZI WA MASHINE YA ULTRA SOUND

Jeshi la Polisi Mkoni Simiyu linawashikilia watu 17 wakiwemo wauguzi wa Hospitali ya mji wa Bariadi kwa tuhuma za kuiba Mashine inayotumika kupima magonjwa ya ndani na kutambua taarifa mbalimbali katika mwili wa binadamu (Ultra sound) katika Hospitali hiyo.

Image result for ultrasound machine

Watu hao wanatuhumiwa kuiba Mashine hiyo pamoja na kifaa chake cha kudurufu picha (printer) ambapo ilikuwa maalumu kwa matumizi ya wodi mpya ya akina mama wajawazito na iliibiwa ikiwa kwenye wodi hiyo.

Kwa mujibu wa Mganga Mkuu wa Halmashauri hiyo, Mike Mabimbi, amekiri kuibiwa kwa mashine hiyo ambapo amesema hadi sasa bado haijapatikana.

Mabimbi amesema kuwa baada ya kutokea kwa tukio hilo waliweza kutoa taarifa jeshi la polisi, ambapo watu 17 wakiwemo wauguzi walikamatwa kwa ajili ya mahojiano.

“Ni kweli mashine hiyo ambayo ilitolewa na wadau wa maendeleo UNFPA kwa ajili ya wodi ya akina mama tu iliibiwa katika mazingira ya kutatinisha, tayari taarifa tulitoa na polisi wanaendelea na uchunguzi,” amesema.

Kwa upande wake Mganga mfawidhi wa hospitali hiyo Mwanaidi Churu, amesema mazingira ya kuibiwa kwa kifaa hicho yameendelea kuwa magumu kutokana na watoa huduma waliokuwepo wodini siku hiyo kila mmoja kudai hajui.