Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 3:35 am

NEWS: WATU 12 WAMEFARIKI DUNIA BAADA YA KUSOMBWA NA MAJI NCHINI BURUNDI

Milli ya watu 12 imepatikana katika maeneo ya Winterekwa na Nyabagere jijini Bujumbura nchini Burundi, baada ya kusombwa na mafuriko makubwa kutokana na mvua inayoendelea kunyesha nchini humo.

Maafisa jijini Bujumbura wanasema mbali na vifo hivyo, watu wengine wamejeruhiwa huku makaazi 21 yakiharibiwa kutokana na mvua hiyo kubwa.

Kuna wasiwasi kuwa huenda idadi ya vifo ikaongezeka na madhara makubwa kushuhudiwa iwapo mvua itaendelea kunyesha na hatua za dharura kutochukuliwa.

Burundi ni miongoni mwa mataifa ya Afrika Mashariki na Kati ambayo yameendelea kushuhudia kiwango kikubwa cha mvua ambacho kimesababisha madhara ikiwemo maafsa.

Mwezi huu wa Desemba, watu zaidi ya 200 wamepoteza maisha katika ukanda huo, kutokana na mvua na maelfu kuyakimbia makwao, nusu ya watu walioangamia wakiwa kutoka Kenya.

Mabadiliko ya tabia nchi, yanaelezwa kuwa chanzo cha kiwango hiki kikubwa cha mvua.