- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WATATU WAKAMATWA KWA KUMUIBIA RAIS MUGABE SH. MILIONI 330
Taarifa kutoka nchini Zimbabwe zinasema kuwa Watu watatu wamefikishwa mahakamani , wakishtakiwa kwa kosa la kuiba mkoba uliokuwa na dolla $150,000 (£117,600) pesa taslimu ambazo zilikuwa mali ya rais wa zamani wa nchini hiyo Robert Mugabe.
Washukiwa hao wa wizi wanadaiwa kutumia pesa hizo kununua magari, nyumba na mifugo.
Jamaa wa rais huyo wa zamani, Constantia Mugabe, ni miongoni mwa walioshtakiwa, kwa mujibu wa taarifa katika vyombo vya habari vya serikali.
Mwanamke huyo anadaiwa kuwa na funguo za nyumba ya kijijini ya Bw Mugabe iliyo eneo la Zvimba karibu na mji mkuu wa Harare, na ndiye aliyewasaidia hao wengine kuingia humo na kufika ulikokuwa mkoba huo.
Washukiwa hao wengine walikuwa wameajiriwa kama wafanyakazi wa kufagia na kusafisha nyumbani humo wakati wa kutekelezwa kwa wizi huo siku moja kati ya tarehe 1 Desemba na mapema Januari.