Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 3:47 pm

NEWS: WATANZANIA 2 WAKAMATWA KENYA WAKIUZA DHAHABU FEKI

Raia wawili wa kutoka nchini Tanzania ni miongoni mwa washukiwa kadhaa waliokamatwa kwa tuhuma za kuuza dhahabu feki nchini Kenya, kisa ambacho kimemkasirisha vikali Rais wa nchi hiyo Uhuru Kenyatta.

Related image

Washukiwa hao walikamatwa na mamilioni ya dola na dhahabu feki kufuatia msako mkali unaofanywa nchini humo kuwasaka wafanyibishara huyo haramu.

Katika msako huo Wengine waliokamatwa ni pamoja Mnigeria na Mcongo mmoja pamoja na wenyeji wao wanne ambao ni raia wa Kenya.

Kwa mujibu wa Shirika la habari la NTV ya Kenya limeripoti kuwa Jumatatu iliyopita kikosi cha polisi wa dharura kilivamia nyumba moja eneo Kileleshwa jijini Nairobi na kukamata dhahabu feki na magari manane na washukiwa wanane.

Vitu vingine pia vilikamatwa katika nyumba hiyo iliyokuwa ikilindwa na maofisa wa usalama.

Mkuu wa idara ya Upelelezi wa Jinai (DCI) George Kinoti alizishauri balozi zote nchini humo kuwatahadharisha wananchi wao kuhusu jambo hilo.