- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WATANO WAHUKUMIWA KIFO KESI YA JAMAL KHASHOGGI
Mahakama nchini Saudi Arabia imewahukumu adhabu ya kifo watu watano kutokana na mauaji ya mwanahabari mkosoaji Jamal Khashoggi ya mwaka wa 2018 mjini Istanbul.
Mwendesha mashitaka mkuu wa Saudi Arabia amesema watu wengine watatu wamepewa vifungo vya jumla ya miaka 24.
Amesema Saud al-Qahtani, mshauri wa zamani wa ngazi ya juu wa Mwanamfalme wa Saudi Arabia, alichunguzwa lakini hakushitakiwa na akaachiwa huru.
Khashoggi, alikuwa mkosoaji kinara wa serikali ya kifalme ya Saudia aliuawa ndani ya ofisi ndogo ya ubalozi wa nchi hiyo katika Jiji la Istanbul, Uturuki mwaka 2018.
Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Saudia amesema mauaji hayo yalikuwa ni sehemu ya "operesheni haramu" na kuwashtaki watu 11 ambao hata hivyo majina yao hayakuwekwa wazi.
Mtaalamu wa Umoja wa Mataifa (UN) alifikia hitimisho kuwa yalikuwa "mauaji ya serikali yasiyofuata utaratibu."
Mtaalamu huyo Agnes Callamard pia alipendekeza kwenye ripoti yake kuwa Mwanamfalme Mohammed bin Salman achunguzwe kutokana na mauaji hayo.
Bin Salman hata hivyo amekanusha kuhusika kwa namna yeyote ile, lakini mwezi Oktob mwaka huu akasema kuwa "anawajibika moja kwa moja akiwa kama kiongozi wa Saudia, na hususani kwa kuwa mauaji hayo yametekelezwa na maafisa wa serikali ya Saudia."
Shirika la kimataifa la kutetea haki za binaadamu la Human Rights Watch limesema kuwa kesi hiyo haikukidhi viwango vya kimataifa na mamlaka za nchi hiyo "zilizuia njia zote stahili za uwajibikaji".
Mwandishi huyo aliyekuwa na miaka 59 alipofikwa na umauti alikuwa akiishi Marekani na kuandika maoni kwenye gazeti maarufu la Washington Post.
Mara ya mwisho kounekana akiwa hai ilikuwa Oktoba 2, 2018 akiingia kwenye ofisi ndogo za ubalozi wa Saudia ili kuchukua karatasi zake za talaka.
Alikuwa mbioni kumuoa mpezi wake wa Kituruki Hatice Cengiz.