- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WATANO WAFARIKI DUNIA, 2,500 HAWANA MAKAZI MAFURIKO MBEYA
Taarifa kutoka Jijini Mbeya ni kwamba Watu watano wameripotiwa kufariki Dunia na wengine zaidi ya 2,500 hawana makazi wilayani kyela Mkoani Mbeya, kusini magharibi mwa nchi kutokana na mvua kubwa zinazoendele kunyesha tangu juzi usiku.
Katika wilaya ya kyela,eneo hili kimsingi linalopakana na nchi jirani ya Malawi ambapo zaidi ya wakazi elfu mbili na mia tano hawana makazi mpaka sasa, kutokana na mvua kunyesha kwa wingi na kuharibu miundombinu ikiwemo barabara za mji huo.
Kwamujibu wa shirika la habari la AFP limemnukuu afisa tawala wilaya wa Kyela Salome Magambo ni kwamba shule na huduma nyingine zimefungwa kutokana na mvua hizo.
Wilaya ya Kyela inapataka na ziwa Nyasa na nchi jirani ya malawi na ni mojawapo ya maeneo yanayopokea mvua nyingi nchini hapa
Mapema wiki hii watu wawili waliripotiwa kupoteza maisha jijini Dar es Salaam kutokana na mvua kubwa zilizonyesha wiki hii.
Maeneo mengi hapa nchini ikiwemo ukanda wa pwani kama Dar es salaam, Tanga, Mkoani Pwani na Morogoro kwa sasa yanashuhudia mvua kubwa huku wataalamu wa hali ya hewa katika taifa hilo wakionya mamlaka kuchukua tahadhari zaidi.