Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 7:46 pm

NEWS: WASOMI ZITTO NA BENSON BANNA WAZUNGUMZIA SAKATA LA MCHANGA WA MADINI

Dar es salaam: Sakata la mchanga wa madini(makinikia) hapa nchini limechukua taswira mpya baada ya wadau na wasomi mbalimbali kuwa na maoni tofauti juu ya sakata hili, Jana kupitia kipindi cha mizani cha kituo cha Televisheni cha Azam Tv Mh. Zitto kabwe alikuwa anatoa maoni yake juu ya sakata hilo, Zitto aliulizwa juu repoti kwenye sakata hili la madini ambalo yeye alianza kulipigia makelele kwenye mgodi wa Bhuzwagi tangu huko nyuma "kwa jambo la kwanza ninalo liona kwamba kunauthubutu, kitendo cha Rais kulisemea hili kuunda kamati na matokeo ya kamati kuwafahamisha wananchi, huu ni uthubutu wa hali ya juu sana ambao Rais Mkapa hakuwahi kufanya na Rais kikwete hakuwahi kufanya" Alisema Zitto,

Pia alisema kuwa jambo kubwa zaidi ambalo linapaswa kuwa mjadala huko tuendako kuwa tatizo kubwa sio makenikia, sio mchanga tatizo kubwa zaidi ni mfumo wa unyonywaji wa rasilima zetu za madini, swala la mchanga au swala la makenikia nijambo dogo sana katika muktadha mzima wa mjadala wa namna gani Nchi yetu inafaidika na mambo ya madini" Zitto alisema kuwa watu wameanza kuhoji haya mambo mda mrefu sana kuna chama cha wanasheria wa mazingira LIDS walianza mapema sana wakati wananchi wa Byananhuru wanafukiwa kwenye mashimo, na baadae nasi tulivyo ingia bungeni tulieleza mapambano yale kwenye mkataba wa Bhuzwagi na badae tume ya BOMANI ikawa imeundwa,

Tushukuru sana swala hili la madini limerudi lilikuwa limeshuka kidogo kwa sababu ya gesi, tutumie nafasi tuweze kujadili nini matatizo ya msingi katika sekta nzima ya madini'' alihoji Zitto

Nae Mhadhiri wa chuo kikuu cha Dar es salaam kitengo cha siasa Profesa Benson Banna alisema kuwa "tatizo la msingi si makinikia, tatizo la msingi nikutoweza kuwa si wabunifu kusuka sera ya madini vizuri na sheria yake vizuri hapo ndipo chimbuko la tatizo, haya madini niyetu na nizawadi kwa watanzania lakini wanao kuja kuyachimba na kuyafaidi ni watu wengine na mikataba haisukwi kwa manufaa ya Mtanzania ni kwa manufaa ya muwekezaji, na sio kwenye tasinia ya madini tu hili la mikataba mibovu linagubika kabisa kila sehemu" aliongea Banna