November 26, 2024, 9:52 am
- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WAPINZANI VENEZUELA MATATANI
VENEZUELA: Bunge jipya la Katiba nchini Venezuela limepiga kura kwa kauli moja kuunga mkono viongozi wa upinzani kushtakiwa kwa makosa ya uhaini, kwa tuhuma za kuchochea nchi hiyo ikawekewa vikwazo vya kiuchumi na Marekani.
Agizo hilo linaelezea mashtaka hayo ni ya kihistoria na kusema kuwa wanakusudia kuwashugulikia wale wote wanaokwenda kinyume na matakwa ya raia wa kawaida wa Venezuela.
Rais wa nchi hiyo Nicolas Maduro mara kwa mara amekuwa akiwatuhumu viongozi wa upinzani kuwa upande wa Marekani, nchi ambayo anasema inajiandaa na uvamizi wa kijeshi.
Wiki iliyopita Rais Donald Trump aliamuru vikwazo vipya kwa Venezuela.