Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 1:28 pm

NEWS: WAPENI ELIMU YA KUJIKINGA NA CORONA WANANCHI-DKT.CHAULA.

DAR ES SALAAM: Wananchi wanatakiwa kupewa elimu jinsi ya kujikinga na ugonjwa wa corona ili kuepusha usisambae endapo atatokea muhisiwa wa ugonjwa huo nchini.


Maelekezo hayo yametolewa leo na Katibu Mkuu Wizara ya Afya, maendeleo ya jamii, jinsia, Wazee na Watoto-idara kuu afya Dkt. Zainab Chaula wakati wa mkutano wa kitaifa wa Waganga Wakuu wa mikoa wa kujadili utayari,changamoto na hatua za kukabiliana na tishio la mlipuko wa COVID-19 uliofanyika kwenye ukumbi wa hospitali ya taifa muhimbili tawi la mloganzila jijini hapa.


“Katika mkoa wewe ndio mtaalam namba moja wa afya kwenye mkoa wako hivyo mnatakiwa kushauri viongozi katika kukabiliana na ugonjwa huu”. Alisisitiza Dkt. Chaula

Amesema upatishanaji elimu juu ya kujikinga na maambukizi kwa wananchi ni jambo muhimu sana kwani jamii inapaswa kuwa na uelewa wa pamoja namna ya ugonjwa huo unavyoambukizwa pamoja na dalili zake ili kila rika iweze kuwa na ufahamu na hivyo itasaidia kuepusha magonjwa ya mlipuko yasiingie nchini.


“Kama nchi za afrika hivi sasa hatupo kwenye utayari bali kwenye kukabiliana kwani tuona ugonjwa huu umezikumba nchi zingine, hivyo kama nchi lazima wataalam wote tujiandae kukabiliana na virus hivi vya Corona ili endapo tutapata mgonjwa basi vyanzo vyote vya maambukizi yanatakiwa kudhibitiwa ili usienee.

Naye Naibu katibu Mkuu Ofisi ya Rais-TAMISEMIanayeshughulikia afya Dkt. Doroth Gwajima amesema kuwa kama TAMISEMI wapo tayari kupokea maelekezo na mafunzo yote ya kisekta ili kutimiza lengo tarajiwa la serikali la kudhibiti na kukabiliana ugonjwa huo.


Dkt. Gwajiama amesema kuwa mkutano huu utasaidia waganga wakuu wa mikoa nchini kutoka na mkakati wa pamoja wa namna ya kukabiliana na ugonjwa huu hususan mikoa ya mipakani kama Kagera, Katavi,songwe, Kigoma,kagera pamoja na mikoa mingine ambayo ipo kwenye hatari ya kuingia kwa magonjwa ya mlipuko.

Hata hivyo Naibu katibu mkuu huyo akiwataka waganga wakuu hao kutoa mafunzo kwa wataalam wengine wa chini yao na viongozi wa mikoa na halmashauri ili kwenda pamoja katika kukabiliana na magonjwa wakati wa dharura.