- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WANUSURIKA KUFA KWA AJALI YA ROLI.
DODOMA: Watu watatu wamenusurika kufariki dunia baada ya roli aina ya Scania lilokuwa likitokea nchini Rwanda kuelekea jijini Dar es salaam kupinduka baada ya breki kufeli katika eneo la Air Port mjini Dodoma huku dereva wa gari hilo akikimbilia kusikojulikana
Katika eneo hili la Air Port hapa mjini muakilishi imeshuhudia idadi kubwa ya wananchi wakishangaa ajali hiyo huku vikosi mbalimbali vya ulinzi na usalama vikiendeleo kuimarrisha ulinzi ambapo kikosi cha zimamoto na uokoaji kilikuwa kikiendelea na jitihada mbalimbali za uokozi
Akizungumza mara baada ya kupokea majeruhi wa Ajali hiyo mganga Mfawidhi wa hospitali ya mkoa Dk Caroline Damian amesema wamepokea majeruhi wawili hospitalini hapo na wote wanaendelea vizuri kutokana na kupatiwa matibabu.
Mmoja wa majeruhi katika ajali hiyo aliyekuwa akipatiwa huduma katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma akaeleza namna ajali ilivyotokea huku akisema kuwa gari hilo lilifeli breki baada ya kukutana na kona kali
Katika eneo la tukio baadhi ya mashuhuda walioshudia ajali hiyo wakaelezea namna ajali hiyo ilivyotokea na kusababisha madhara ikiwemo moja ya nyumba iliyopo karibu na eneo la barabara hiyo kudhurika
Muakilishi imezungumza na Mkuu wa kituo cha zimamoto mkoani Dodoma Amir Msengi ambaye alifika eneo la tukio ambapo amesema baada ya kupata taarifa za ajali hiyo walifika eneo la tukio na kusaidia kuokoa w waliokuwepo kwenye ajali hiyo huku akiwataka madereva kuwa makini wanapokuwa na vyombo vya moto
Baadhi ya majirani wanaoishi karibu na eneo lilipotokea ajali hiyo wameiomba serikali kuweka alama za barabarani zitakazowasaidia madereva kutambua eneo hilo kuwa lina kona kali kwani imekuwa ikisababisha ajali za mara kwa mara
Ajali za barabarani zimekuwa zikisababisha ulemavu wa kudumu,majeraha na wengine wamekuwa wakipoteza ndugu jamaa na marafiki hivyo kuna kila sababu ya kupambana na Ajali za barabarani zinazogharimu maisha ya watu