- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
News: Wanawake wajengewa uwezo katika masuala ya uongozi
DODOMA: Wanawake wametakiwa kujitokeza katika kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi Mkuu na chaguzi nyingine zinapotangazwa.
Akitoa mada ya uongozi katika mafunzo yaliyoandaliwa kwa ajili ya kuwajengea uwezo wanawake wa jijini hapa,Mratibu na mwezeshaji wa mradi huo kutoka shirika lisilo la Kiserikali na kutetea haki za mwanamke (WOWAP) Leonard Konjani alisema, lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea na kuwaongezea wanawake uwezo katika masuala ya uongozi.
“Tunaamini kwa kutoa mafunzo haya ,wanawake wataweza kushiriki katika shughuli na nyadhifa mbalimbali za uchaguzi wakiwa wamejengeka katika maadili ya uongozi na hatimaye kuweza kutimiza majukumu yao vyema pindi watakapogombea na kupata nyadhifa hizo.”amesema Konjani.
Amesema WOWAP iliamua kutoa mafunzo hayo kwa wanawake baada ya kuonekana kundi hilo kutopewa nafasi huku akisema hiyo ni fursa pekee ya kuwajenga kiuwezo katika masuala ya uongozi ili waweze kufikia idadi ya uwiano wa kijinsia kati yao na wanaume ya 50 kwa 50 katika nafasi za uongozi.
“Lakini pia tunaiunga mkono Serikali katika juhudi za kulisaidia kundi hili la wanawake katika kufikia 50 kwa 50.Amesema Konjani
Konjani alisema kutokuwepo kwa usawa kati ya wanawake na wanaume katika masuala ya kiungozi ni miongoni mwa changamoto zinazolikabili kundi la wananwake ambapo wanahitaji kupata elimu na mafunzo ya kutosha ili waweze kuwa na uthubu.
Aidha ameziasa kamati zenye wajibu katika chaguzi mbalimbali kuhakikisha zinatoa kipaumbele hasa kwa kundi la wanawake lakini pia kuwaondolea vikwazo ili washiriki na kupata nafasi kama ilivyo kwa wanaume.
Awali akifungua mafunzo hayo Afisa Maendeleo wa Jiji la Dodoma Peter Malya aliwataka wanawake kushiriki katika ngazi zote za maamuzi bila kuwa woga wowote.
Alilitaka kundi hilo pia kuhakikisha linakuwa na deststuri ya kuwaunga mkono kwa kuwapigia kura ya ndio wanawake wenye uwezo na wanaojitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi.
“Mafunzo haya yabadilishe mitazamo hasi kati ya mwanamke na mwanamke hasa kwenye ushiriki wa masuala ya uongozi”alisema Malya
Mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo Penina Kaminyoge alisema,mara nyingi wanawake wamekuwa wakijitokeza kugombea nafasi mbqlimbali za uongozi katika chaguzi mbalimbali lakini wengi wao wamekuwa wakikatwa majina bila sababu za msingi.
“Hii kwa kweli imekuwa ikiwatisha tama wanawake wengi,tunaziomba kamati za uchaguzi ziwe na msimamo na kutoa haki kwa kila mgombea .”alisema Penina
Mradi huo wa kuwajengea uwezo w wanawake katika masuala ya kiuongozi umefadhiliwa na Canada Fund for Local Initiative (CFLI ) na kutolewa na WOWAP.