- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WANAWAKE WAIBUKA KINARA MATOKEO KIDATO CHA SITA 2017
DAR ES SALAAM: Bora wa ufaulu kwa wanafunzi wa kidato cha sita kwa mwaka 2017 kimepanda kwa asilimia 0.59 ikilinganishwa na mwaka jana, huku wasichana wakifanya vizuri zaidi ikilinganishwa na wavulana
Kwa kuzingatia madaraja waliyoyapata watahaniwa wa shule, jumla ya watahiniwa 58,556 ambao ni sawa na asilimia 93.72 wamefaulu katika daraja la kwanza hadi la tatu. Kwa mujibu wa Baraza la mitihani la taifa (NECTA),ufaulu huu unajumuisha wasichana 22,909 ambao ni sawa na asilimia 94.07 na wavulana 35,647 ambao ni sawa na asilimia 93.49.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa Dk. Charles Msonde ameeleza kuwa idadi ya watahaniwa waliopata daraja la kwanza hadi la tatu katika mwaka 2017 imepanda kwa asilimia 0.59 kutoka asilimia 93.13 ya mwaka 2016 hadi asilimia 93.72 ya mwaka huu.
Kwa matokeo haya, wasichana wamefanya vizuri zaidi ikilinganishwa na wavulana. Akifafanua ufaulu huo, Dk. Msonde amesema kwamba wasichana (22, 909) wamefaulu kwa asilimia 94.07 ikilinganishwa na asilimia 93.49 ya wavulana 35,647.
Shule za Feza Girls, Marian Boys ya Pwani, Kisimiri (Pwani), Ahmes (Pwani), Marian Girls(Pwani), Mzumbe(Morogoro), St. Mary(Mazinde Juu), Tabora Boys(Tabora), Fedha Boys(Dar es Salaam) na Shule ya Kibaha ndizo zilizofanya vizuri katika masomo yote.Shule hizo zote zinaonesha kuwa na idadi ya watahiniwa chini ya 200.
Kwa mujibu wa NECTA, shule ya Feza Girls ilikuwa na watahiniwa 67, wakati Marian Boys(94), Kisimiri(58), Ahmes(40), Marian Girls(108), Mzumbe(144), St. Mary Mazinde Juu(149), Tabora Boys(129), Feza Boys(86) na Kibaha(173).
Mbali na ufaulu mzuri wa jumla kwa wasichana, pia wamefanya vizuri katika masomo ya saysani kwa kushika nafasi mbili za mwanzo. Wanafunzi hao ni Sophia Juma wa shule ya St Mary Mazinde juu kutoka Tanga na Agatha Ninga kutoka shule ya Tabora Girls.
Wanafunzi wengine waliofanya vizuri katika kumi bora ni pamoja na Nathanael Ndagiwe kutoka Mzumbe, Mugisha Lukambuzi kutoka Feza Boys ya Dar-es-Salam,Innocent Labule kutoka St.Mary Goretina Masaba kutoka Kibaha.
Wengine ni Arsen Mwanyuke kutoka Marian Boys, Atuganile Cairo kutoka Feza Girls na Erick Philipo kutoka Kibaha. Aidha, shule kumi ambazo zimefanya vibaya kwa kushika nafasi za chini katika matokeo hayo ni pamoja na Kiembesamaki ya Unguja, Hagafilo(Njombe),Chasani(Pemba), Mwenyeheri Anuarite(Dar-es-Salaam), Ben Bella(Unguja), Meta(Mbeya),Mlima Mbeya, Njombe pamoja na shule ya Al-ihsani Girls ya Unguja na St.Vicent ya Tabora.